Ticker

10/recent/ticker-posts

RC Senyamule amlilia Hayati Rais Mwinyi ,asema ametuachia mengi ya kujifunza kama Viongozi


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule amesema Tanzania itamkumbuka kwa kuenzi mema na mazuri mengi yaliyofanywa na Rais wa awamu ya pili nchini Tanzania Hayati Ali Hassan Mwinyi aliyefariki Dunia wiki iliyopita na kuzikwa nyumbani kwake Kisiwani Unguja,Zanzibar 

Mhe.Senyamule pichani akiwa  na viongozi mbalimbali walioshiriki katika mazishi ya Hayati Rais Ali Hassan Mwinyi yaliyofanyika kwa itifaki za kitaifa alisema hakuna asiyejiu mchango wa Marehemu Rais Mwinyi katika nchi yetu.

“Kama mnavyofahamu nchi yetu imempoteza mmoja wa viongozi wake mahiri ambaye aliwahi kuwa Rais wa awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi ambapo kwetu kama viongozi lazima tuyaenzi maisha na mema aliyoyafanya mzee wetu huyu 

Alimalizia RC Senyamule huku akionekana mwenye Huzuni mjini Unguja.

Post a Comment

0 Comments