Wataalamu wa Benki ya Dunia wameelezea kuridhiswa kwao na utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji wa Barabara za Vijijini kwa Ushirikishaji na Ufunguaji wa Fursa za Kijamii na Kiuchumi (RISE) unaotekelezwa na Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) ambapo wamesema moja ya sababu za matokeo hayo ya utekelezaji yanatokana na usimamizi mzuri wa kazi pamoja na timu nzima ya Utekelezaji.
Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Mhandisi Victor Seff (pichani) akizungumza katika kikao kazi hicho ameishukuru Benki ya Dunia kwa kuendelea kufadhili miradi mbalimbali ya Barabara inayotekelezwa chini ya TARURA Nchini.
Akizungumza katika kikao hicho mratibu wa Miradi ya Benki ya Dunia toka TARURA Mhandisi Haumprey Kanyenye (mwenye tai nyeusi) amesema Mradi wa RISE ulianza Novemba 2021 na utakamilika Juni 2027. Mradi wa RISE umelenga kujenga jumla ya kilometa 535 za barabara kwa kiwango cha lami, kujenga maeneo korofi ya barabara ili yapitike, na kufanya matengenezo ya barabara ya jumla ya kilometa 23,000km kwa kuwashirikisha wananchi wanaoishi pembezoni mwa barabara husika . Aidha, Mhandisi Kanyenye alieleza uchaguzi wa Mikoa, Wilaya na barabara ambapo Mradi wa RISE unatekelezwa ulizingatia maeneo yenye uzalishaji mkubwa wa mazao ya kilimo kutoka kwenye Mpango wa Maendeleo wa Kilimo (ASDPII).
Akiongea katka kikao hicho Focal Person wa masuala hayo ya unyanyasaji wa Kijinsia Sr.Eutropia Eugen amesema wao kama wawakilishi wa TARURA wanamshukuru Mtendaji Mkuu kwa wa TARURA Mhandisi Victor Seff kwa kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanakamilisha majukumu yao kwa mujibu wa sheria na ameahidi ataendelea kuhakikisha wanatoa Elimu kwa jamii ya masuala hayo ya jinsia pamoja na elimu kuhusu jamii kujikinga na virusi vya (STD's) na (HIV -AIDS) kwenye Eneo la Miradi ili kuunga Mkono jitihada za Serikali inayoongozwa na Mhe.Samia Suluhu Hassan kuhakikisa jamii inaelimika kwenye nyanja mbalimbali hasa katika maeneo hayo yenye miradi ya maendeleo ikiwepo inayotekelezwa na wafadhili mbalimbali.
0 Comments