Ticker

10/recent/ticker-posts

Mtendaji Mkuu TARURA na Mbunge Sichwale wakagua Ujenzi wa Daraja la Msagano na Kivuko Wilaya ya Momba - Songwe



Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mhandisi Victor H. Seff pamoja na Mbunge wa Jimbo la Momba Mhe. Condester Sichwale walipotembelea Ujenzi wa Daraja la Msangano lililopo katika Wilaya ya Mombo Kijiji cha Msangano Halmashauri ya Wilaya ya Momba. 


Utekelezaji wa ujenzi wa Daraja la Msangano umeanza mwaka wa fedha 2023/2024 na utakamilika baada ya miaka miwili. Aidha, Mtendaji Mkuu alimtaka Mkandarasi kuharakisha ujenzi wa Daraja hilo kwa muda uliopangwa katika mkataba. Aidha, ziara hiyo ilitokana na ahadi aliyoitoa Mtendaji Mkuu kwa Wananchi wa Msangano pindi alipofanya ziara tarehe 28/09/2023 na kuwaahidi baada ya mwezi mmoja Mkandarasi ataanza kazi za ujenzi wa Daraja na atarudi tena baada ya miezi miwili kujione maendeleo ya utekelezaji.

Pia katika ziara yake hiyo ya kukagua miradi inayotekelezwa na TARURA Wilayani Momba Mkoani Songwe Mtendaji Mkuu huyo alitembelea Ujenzi wa Kivuko cha Kiteputepu cha Nsanzya kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Momba. 

Akielezea na kuishukuru Serikali inayoongozwa na Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuipa TARURA Fedha za utekelezaji wa Miradi ya ya maendeleo na ile ya Kimkakati Mhe. Condester Sichalwe Mbunge wa Jimbo la Momba (mwenye Kofia) Amempongeza Mtendaji Mkuu wa TARURA kwa kuwa mfatiliaji mzuri wa utekelezaji wa Miradi huku akimueleza Mtendaji Mkuu adha wanayopata wananchi wa vijiji vitatu (3) vya Nsanzya, Chuo na Kahonga kushindwa kusafirisha mazao yao. 

Aidha,  Mhe. Mbunge aliomba ujenzi wa Daraja la kupitisha Magari ufanyike ili kurahisisha usafiri wa Mazao yanayolimwa kwenye Vijiji hivyo jambo ambalo maombi hayo yamepokelewa na Mtendaji Mkuu wa TARURA kwa ajili ya kuyafanyia kazi kulingana na Upatikanaji wa Fedha.


Post a Comment

0 Comments