Ticker

10/recent/ticker-posts

MPYAA: Mawaziri Anthony Mavunde na Jerry Silaa wakutana LIVE kwenye Kliniki hii kubwa Dodoma Leo.


 Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry William Silaa akiwa pamoja na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe. Anthony Peter Mavunde wakati wa Kliniki ya usikilizaji na utatuzi wa migogoro ya Ardhi kwa wananchi wa Dodoma Jiji.
 
Mamia ya Wananchi wa Jiji lla Dodoma wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe.Anthony Mavunde waliofika leo asubuhi katika Kliniki Maalum ya Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi iliyoanzishwa na Waziri wa Wizara Hiyo Mhe.Jerry Silaa kwa ajili ya Kuhakikisha wanasikilizwa na kutatuliwa shida zao zinazotokana na migogoro ya Ardhi ambapo Kliniki hiyo imeonyesha mafanikio makubwa mpaka sasa.
Waziri Silaa akiwa na Katibu Mkuu wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ndugu Sanga wakimsikiliza mmoja wa wananchi wa Dodoma waliofika katika Kliniki hiyo leo Asubuhi.
Waziri wa Madini na Mbunge wa Dodoma Mjini Mhe .Anthony Mavunde  akimsikiliza mmoja wa wananchi wa Dodoma waliofika katika Kliniki hiyo leo Asubuhi kutatuliwa moja ya shida za migogoro ya ardhi ambapo Mbunge Mavunde ameahidi kuwasaidia wananchi wake kuhakaikisha wanapata utatuzi wa Migogoro hiyo.







Post a Comment

0 Comments