Ticker

10/recent/ticker-posts

RC ROSEMARY SENYAMULE AFUNGUKA HAYA KUHUSU MECHI YA YANGA NA USM ALGIERS KESHO ,...AWATAKA WATANZANIA KUWA WAZALENDO

Mkuu wa mkoa wa  Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule amekuwa mstari  wa  mbele katika kuunga mkono juhudi za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan za kuinua  michezo nchini kwa kuwapa motisha klabu za Simba na Yanga  waliokuwa katika mashindano Makubwa ya kimataifa ya Klabu bingwa na kombe la shirikisho barani Afrika.

Aidha Mhe.Senyamule amewapa salamu za kuitakia ushindi klabu ya Yanga kesho 28/05/2023 katika mchezo wa kwanza wa fainali ya Kombe la Shirikisho La soka CAF barani Afrika dhidi ya Timu ya USM Algiers ya Algeria utakaochezwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Mhe.Senyamule ameenda mbali zaidi kwa kuwataka mashabiki wote wa soka nchini bila kuangalia vilabu vyao kuishangilia timu ya yanga ili kumuunga mkono Mhe.Rais Samia katika kuinua michezo kwa kuitakia ushindi Yanga ambapo amesema ushindi wa Yanga hapo kesho ni muhimu sana na ni ushindi wa watanzania wote kwani Yanga inawakilisha Nchi  na kuwataka mashabiki waweke uzalendo mbele kwa maslahi mapana ya Taifa kwa kuunga mkono juhudi hizo za Mhe.Rais Samia za kuhakikisha anaona sekta ya michezo inainuka nchini.



Post a Comment

0 Comments