Ticker

10/recent/ticker-posts

Hii ndiyo taarifa ya Majeruhi Katika Ajali ya Kukanyagana Uwanja wa Mkapa jijini Dar jana.

 

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Balozi Dkt. Pindi Chana akiwa ameongozana na Naibu Waziri wake, Hamis Mwinjuma maarufu @mwanafa, Katibu Mkuu, Saidi Yakubu, RC Chalamila na DC wa Temeke, Mwanahamisi Munkunda kwa pamoja wamewajulia hali majeruhi 10 wanaoendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya Temeke waliojeruhiwa kutokana na tukio la kukanyagana katika Mkapa Stadium wakati wakijiandaa kuingia uwanjani kutazama mechi kati ya Yanga na USM Alger ya nchini Algeria katika mchezo wa Kwanza wa Fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Chana amepokea taarifa kutoka kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Joseph Gasper Kimaro ambapo amesema walipokea majeruhi 30 wakiwemo Wanaume 18, Wanawake 10 na Mtoto Mmoja ambapo mgonjwa mmoja alipoteza maisha wakati akipatiwa matibabu.

Mpaka sasa Wagonjwa wengine wameruhusiwa na wamebakiwa na Wagonjwa 10 na wote wanaendelea kupatiwa matibabu na hali zao zinaendelea kuimarika.

Post a Comment

0 Comments