Shule za sekondari zilizoshiriki katika kambi hiyo ya Ubunifu ni Pamoja na Arusha Science Secondary,Kilasara Secondari ,shepherd Secondary na nyinginezo.
Mratibu wa Mafunzo kutoka shirika la The Foundation For Tommorow Evelyn Kaijage amesema kuwa ushirikiano na shirika la ndege la Boeing kutoka Marekani unalenga kuwawezesha vijana kushiriki katika masomo ya sayansi na kufanya tafiti na buniifu ambazo zitasaidia kutatua changamoto zilizoko katika bara la Africa.
Evelyn ameongeza kuwa ufadhili wa Boeing na JA Africa utasaidia kupata idadi kubwa ya wanafunzi wa kike kupenda masomo ya sayansi na kuwezesha kupata wataalamu waliobobea katika masuala ya sayansi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Juniour Achievement Africa (JA) Phil Mlambo amepongeza shirika la Boeing kwa kuwasaidia wanafunzi wa masomo ya sayansi kuwaza kibunifu Zaidi na kufikiria kutatua changamoto zinazoikabili jamii yao kupitia bunifu zao.
Kwa Upande wao wanafunzi walioshiriki kwenye kambi hiyo ya ubunifu akiwemo Elizabeth Cathbet kutoka Shule ya sekondari Arusha Science amesema kuwa kambi hiyo imewawezesha kupata uzoefu na maarifa kutoka kwa wabunifu mbali mbali na wanasayansi ili kuongeza ari ya wao kujikita Zaidi kwenye sayansi na ubinifu.
Asimwe Elly ni Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Kilasara kutokana na mwamko mkubwa wa masuala ya sayansi inaotokana na juhudi za TFFT tayari wameanza kubuni teknolojia mbali mbali ambazo zinahitaji ulinzi wa kisheria ili ziweze kuwanufaisha wabunifu.
0 Comments