Ticker

10/recent/ticker-posts

AFYA: MAGONJWA YA MOYO – AINA, CHANZO, DALILI, TIBA

  


UTANGULIZI – YAJUE MAGONJWA YA MOYO

Magonjwa ya Moyo ni magonjwa yanayoambatana na kuathiri moyo. Mara nyingi magonjwa ya moyo yanaambatana na mishipa ya damu kuwa na tatizo ambapo moyo hushindwa kufanya kazi, moyo hutegemea damu ambayo hubeba oxygen, madini, vitamins, kinga ya mwili, joto, homoni na vingine vingi.

Kwa mwaka 2015 pekee zaidi ya watu milioni 17.7 walifariki kutokana na magonjwa ya moyo na mfumo wa damu. Hii ni sawa na theluthi ya vifo vyote duniani. Zaidi ya theluthi ya vifo vyote vinavyotokana na ugonjwa wa moyo na mishipa ya damu hutokea ndani ya nchi zenye uchumi wa chini na uchumi wa kati


AINA ZA MAGONJWA YA MOYO

Zipo aina mbalimbali za magonjwa ya moyo hutofautiana japo yote huathiri moyo, nayo ni;

Ugonjwa wa moyo unaotokana na kuathirika kwa mishipa ya damu (Coronary artery disease) Hili ni tatizo linalowakuta watu wengi, mishipa ya damu hupasuka na kuharibika hii hutokana na mishipa ya damu kuwa na uchafu na mafuta mengi na kufanya damu isipite vizuri

Mapigo ya moyo kwenda tofauti (Heart Arrhythmias) Hii hutokea pale mapigo ya moyo kwenda taratibu isivyo kawaida au kwenda haraka isivyo kawaisda, pia mapigo ya moyo kwenda ovyo. Hii ni hatari sana na huua sana

Moyo kushindwa kufanya kazi (Heart Failure) Hii ni hali moyo hushindwa kufanya kazi yake kama kupampu na kusambaza damu, kusambaza oxygen. Hii inaweza kutokea kwa mtu mwenye magonjwa kama ugonjwa wa moyo wa misipa kuathirika, Shinikizo la damu, na magonjwa mengine

Magonjwa ya moyo ya kuzaliwa (Congenital heart disease) Haya ni magonjwa ambayo wengi huzaliwa nayo, yanaweza kuwa ni baadhi ya kasoro katika mwili kama baadhi ya chemba za moyo kuziba au kupasuka, oxygen kupita kwa shida na vinginevyo.

Ugonjwa wa valvu na misuli ya moyo (Heart Valve Disease & Cardiomyopathy (Heart Muscle Disease)) Katika moyo kuna chema nne nazo zinapitisha damu na  oxygen kutoka kwenye mapafu, valvu hufunguka na kufunga. Valvu na misuli ikiwa imepasuka na kuharibika husababisha tatizo la moyo.

Moyo kutanuka. Hii hutokea pale damu ikiingia ndani ya moyo harafu mishipa ya kutoa damu ikiwa na tatizo ikashindwa kutoa damu nje ya moyo moyo utaanza kutanuka siku hadi siku. Kutanuka kwa moyo kunatokea usipotibu baadhi ya matatizo kama shinikizo la damu, moyo kwenda mbio, valvu na misuli ya moyo n.k.

BONYEZA HAPA ENDELEA KUSOMA

Post a Comment

0 Comments