Ticker

10/recent/ticker-posts

TARURA WAENDELEA NA KASI YA UJENZI WA BARABARA ZA LAMI KILA KONA...SOMA ZAIDI HAPA

Na Cresensia Kapinga wa JamhuriMedia,Songea

JUMLA ya sh.milioni 389.8 zimetolewa na wakala wa barabara za mijini na vijijini(TARURA),Manispaa ya Songea,kujenga ujenzi wa boksi karavati na barabara ya rami kwa kiwango chepesi 0.71cm yenye urefu wa mita 700 ikiwa ni mwendelezo wa ujenzi wa barabara ya Tunduru JCT -Seedfarm yenye lengo ya kuwaondolea adha wananchi ya vumbi kujaa kwenye nyumba zao,matope na mifereji kuziba msimu wa mvua.
Akizungumza na wanahabari hivi karibuni  Kaimu Meneja Wakala wa Barabara za mijini na Vijijini (TARURA), Wilaya ya Songea,Mhandisi Johson Kweka (Pichani Juu)amesema mradi huo unajengwa na mkandarasi M/S OVANS Construction LTD Mbinga,Kwa gharama ya sh.389,834,800 ulianza rasmi Agosti 18, mwaka huu, na unatarajia kukamilika Desemba 16, mwaka huu.

Kwa kuongezea mwandishi wetu alimpigia simu Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seff ili kujua ana maoni gani kuhusu ujenzi wa barabara hiyo ambapo alisema TARURA inajenga barabara Vijijini na Mijini  kulingana na mahitaji ya kila eneo ingawa utekelezaji wa miradi ya lami nyepesi na nyinginezo utatekelezwa  kadri fedha zinavyopatikana lakini pia pamoja na hayo amesisitiza ubora zaidi katika kazi jambo ambalo yeye amejipambanua kwa kusema yeye haweza kumvumilia mkandarasi aiyetimiza ubora unaotakiwa.

Post a Comment

0 Comments