Ticker

10/recent/ticker-posts

TANZIA: Rais Mstaafu Mkapa amefariki Dunia “tulipokee hili, msiba mkubwa”

Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ametangaza kifo cha aliyekuwa Rais wa awamu ya tatu Benjamin William Mkapa ambae amefariki wakati akiwa anapatiwa matibabu Hospitali Jijini Dar es salaam.
“Mzee wetu Benjamin William Mkapa, Rais wa Awamu ya Tatu amefariki Hospitali DSM ambako alikuwa amelazwa, Watanzania tulipokee hili, tumepata msiba mkubwa na tuendelee kumuombea Mzee wetu ambaye ametangulia mbele ya haki”- JPM