Ticker

10/recent/ticker-posts

Rais Magufuli amkaanga kigogo TAKUKURU “mnajipendekeza kwangu, nitakuvua nyota, unajengaje ofisi Chato”


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli amewataka Viongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU kuacha kujipendekeza kwake na wafanye kazi.

“Mjipendekeze Chato wakati nimeshaondoka kwenye Urais, Chato wana Ofisi ya TAKUKURU, mnajenga nyingine yanini? au ulifikiri nitafurahi ukisema Chato? mimi moyo umeshakuwa Sugu, Spika anasema hakuna Ofisi Kongwa hiyo mliyotaka kujenga Chato mkajenge Kongwa” -JPM

“Mnasema mnataka kujenga Ofisi ya TAKUKURU Chato nawashangaa, TAKUKURU Chato tuliwapa Jengo tena la ghorofa lipo juu milimani kwenye shamba la Marehemu Baba yangu akanyang’anywa, msizungumze mambo kwa kunifurahisha mimi na kujipendekeza this is not the way”-JPM