Ticker

10/recent/ticker-posts

Rais Kenyatta aguswa na msiba wa Mstaafu Mkapa

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ametuma ujumbe wa salamu za pole kwa Rais wa Tanzania, John Magufuli; Watanzania wote pamoja na familia kufuatia kifo cha Rais Mstaafu Benjamin Mkapa.
Katika ujumbe wake, Rais Kenyatta amemuomboleza kiongozi huyo kama mtu bora wa Afrika Mashariki aliyefanya kazi kwa bidii kwa ajili ya amani na maendeleo ya Kanda ya Afrika Mashariki.
Rais Kenyatta ameitakiwa familia ya Rais huyo Mstaafu na Watanzania wote kwa ujumla faraja kutoka kwa Mungu wakati huu wa kuomboleza kuondokewa na Kiongozi wao.
Benjamin William Mkapa aliyefariki usiku wa kuamkia leo hospitalini alikokuwa amelazwa alikuwa Rais wa Tanzania kuanzia mwaka 1995 hadi mwaka 2005 kupitia chama cha CCM.