Ticker

10/recent/ticker-posts

WAZIRI KAMWELE AKABIDHI ENEO LA KIWANJA KWA AJILI UJENZI WA MAKAO MAKUU YA MASHIRIKA YA POSTA AFRIKA

 Waziri wa ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe  akimuonyesha mkandarasi  ramani ya jengo hilo la makao makuu ya Mashirika ya Posta Afrika ,jengo hilo linatarajiwa kuwa na ghorofa 16  na linatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 30 (picha na Woinde Shizza,Arusha)

  Waziri wa ujenzi ,uchukuzi na Mawasiliano Muhandisi Isack Kamwelwe akimuelekeza mkandarasi eneo LA uwanja lililopo jiji Arusha kwa ajili ya ujenzi Wa jengo LA  makao makuu ya mashirika ya posta Kwa nchi za Afrika ,litakalo gharimu kiasi cha shilingi za kitanzania Bilioni 33 (picha na Woinde Shizza,Arusha).

 Msimamizi na mshauri wa ujenzi wa jengo hilo  Nathanael Alute  kutoka kampuni ya B.J. Amuli  Architects akitoa maelezo mbele ya Waziri Kamwelwe.
 Mkandarasi  wa kampuni ya Beijing Construction Enginering Group  ,Liang  Li akimueleza Waziri Kamwelwe kuwa watakamilisha ujenzi huo Wa jengo LA makao makuu ya mashirika ya posta Afrika kwa wakati (picha na Woinde Shizza,Arusha).
Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Jonathan Shanna akiongea na Waziri  Kamwelwe ambapo alimuhaidi kulinda eneo hilo huku akitoa onyo kwa Mtu  yeyote ambae atakutwa katika eneo hilo bila kibali kuchukuliwa hatua Kali za kisheria

 
 Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

WAZIRI wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano 
Mhandisi Isack Kamwelwe leo Januari 8 mwaka 2020 amemkabithi rasmi kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa jengo la makao makuu ya mashirika ya Posta Afrika.
 
Kwa mujibu wa Waziri Kamwelwe  mkandarasi wa jengo hilo ni Kampuni ya Beijing construction ,Liang Li jengo na litajengwa ndani ya Jiji LA Arusha na litagharimu Sh.bilioni bilioni 30 .

Akizungumza wakati wa kukabidhi eneo hilom  Mhandisi Kamwelwe amesema  ujenzi huo umekuja muda muafaka kwa kipindi cha Rais wa Awamu ya Tano Dk.John Magufuli ambaye  anafata nyayo za Baba Wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na anaamini kuwa ujenzi huo utakamilika kwa wakati

"Kuna nchi 45 wanachama wa mashirika ya Posta katika nchi za Afrika 1980 walikaa na kukubaliana makao makuu ya mashirika ya posta yawe hapa nchini Tanzania na Baba wa Taifa akakubaliana nao na wakapanga yajengwe Arusha na ndio maana katika kuathimisha miaka 40 ya mashirika haya tumeamua tuanze kujenga jengo la makao makuu ya mashirika haya ya posta Afrika" amesema Waziri Kamwele

Amesema jengo hilo litakuwa na gorofa 16 na hadi kumalizika litagharimu kwanba linatakiwa kujengwa na kumalizika kwa kipindi cha miezi 30 huku akimtaka Mkandarasi wa jengo hilo kujenga katika ubora unaotakiwa na viwango vya Serikali .

Amewataka wakandarasi hao kuhakikisha wafanyakazi wao ambao wanatoka nje ya nchi kuja na nyaraka zote za uhamiaji pamoja na vibali vya kufanyia kazi hapa nchini.

"Jengo hilo ni makao makuu ya mashirika ya posta Afrika, hivyo hairuhusiwi mtu yeyote asiehusika kuingia katika eneo hili bila kibali kutoka kwa wahusika ,eneo hili ni la kimataifa halitakiwi kuingia bila kibali iwapo mtu atakutwa hatua kali za kisheria,"amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Dk Jones Kilembe ameishukuru Serikali kwa jinsi ilivyoonyesha usimamizi na ufuatiliaji hadi kufikia hapa tulipofika katika ujenzi wa jengo hilo la makao makuu ya mashirika ya posta Tanzania.

Amewataka wananchi wa Arusha kutoa ushirikiano katika masuala ya  ulinzi hata ikitokea katika eneo la uchangiaji huku akiongeza  kuwa watamsimamia vyema mkandarasi huyo na kuhakikisha anamaliza kazi kwa muda uliopagwa na ikiwezekana hata kabla ya muda uliopangwa kufika

Wakati huo huo Mkuu Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ameishukuru Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kujenga makao makuu ya mashirika ya posta nchi za Afrika jijini hapa.
 
Ambapo amesema  kwa nafasi yake atashirikiana nao vyema katika kutatua vikwazo vyote vilivyopo ndani ya uwezo wake katika nafasi ya ngazi ya mkoa ili kuhakikisha mkandarasi anamaliza Kazi kwa wakati.

Msimamizi na Mshauri Wa jengo hilo Nathanael Alute kutoka kampuni ya B.J. Amuli Architects amesema kuwa atasimamia vyema ujenzi huo uwe wa viwango vinavyotakiwa na serikali ,na kumalizika kwa muda uliopangwa huku akijitaidi gharama za ujenzi zisiwe kubwa zaidi.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/303kCME
via

Post a Comment

0 Comments