Ticker

10/recent/ticker-posts

UJENZI WA MAKAO MAKUU UMOJA WA POSTA AFRIKA ( PAPU) KUANZA RASMI ARUSHA.


Waziri wa ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Injinia Isaack Kamwele akikagua Eneo la kiwanja ambacho kitajengwa jengo la Umoja wa Posta Afrika.wa kwanza kushoto ni mkuu wa kanda ya Kaskazini kuutoka Mamlaka ya Mawasiliano Nchini Mhandisi Imelda Salum.

Waziri wa ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Injinia Isaack Kamwele akiwa amemshika mkono Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe.Mrisho Gambo,akiwa pia anasisitiza jambo kwa baadhi ya watumishi
Waziri Kamwele akibadikishana mawazo na mhadisi mshauri katika Makao makuu ya Pan African Union( Papu)
aziri wa ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Injinia Isaack Kamwele akiteta jambo na mhadisi mshauri katika Makao makuu ya Pan African Union (Papu).



Mkandarasi akionyesha Mhe.Waziri picha ya ramani ya jengo ambalo zitajengwa ofisi za Pan African Union (Papu)

Na.Vero Ignatus,Arusha.


WAZIRI wa Ujenzi,Uchukuzi,na Mawasiliano Mhandisi Isaack Kamwele amekabidhi eneo la makao makuu ya Umoja wa Posta Afrika (PAPU)eneo Hilo lipo mjini Arusha, kwa mkandarasi wa kampuni ya China inayojulikana kwa jina la Beijing Construction Engeneer.

Akizungumza katika makabidhiano hayo yaliyofanyika makao makuu ya (Papu ) Jijini Arusha,Waziri Kamwele alisema kuwa mkandarasi huyo, ambaye ni Meneja wa kampuni hiyo, Li Liang, ahakikishe kuwa Ujenzi wa jengo Hilo unakamilika ndani ya miezi 30 au chini yake ili kuhakikisha kuwa wanatekeleza kwa Wakati na kwa viwango vonavyohitajika.

Aidha alisema kuwa eneo hilo lipo chini ya Umoja wa mataifa hivyo hakuna ambaye anaruhusiwa kuingia Eneo Hilo bila kibali kutoka wizara ya mambo nje na ushirikiano wa Kimataifa.

Amewataka viongozi wa Mkoa wa Arusha akiwepo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Jonathan Shana kuimarisha ulinzi katika Eneo hilo kwaajili ya manufaa ya watanzania na kwa wanaArusha pia.

Ujenzi wa Eneo hilo unafuatiama makubaliano ya Rais wa kwanza wa Tanzania marehemu Julius

Nyerere alitoa eneo hili mwaka 1980, baada ya njia za umoja wa Afrika takribani 54 kupendekeza Makao makuu ya Papu kujengwa mkoani Arusha,hivyo takribani miaka 40 imepita tangu maazimio hayo.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA),Injinia James Kilaba alisema kuanza kwa ujenzi huo ni furaha na fursa kwa watanzania ambapo alitoa wito ujenzi huo ufanywe kwa weledi na kwa kuzingatia mkataba uliopo.

Msimamizi wa mradi huo kutoka kampuni ya B.J.Amuli Architects,Nathanael Alute aliahidi kusimamia ujenzi huo ili ukamilike ndani ya miezi 30 huku akiahidi kuwa atahakikisha kuwa anamshauri mkandarasi kupunguza muda wa ujenzi bila kuathiri ubora.

Katibu Mkuu Msaidizi wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU),Kolawole Raheem Aduloju, alimshukuru Rais John Magufuli kuweka histori kwa kuhakikisha
ujenzi huo unafanyika baada ya miaka mingi kupita.


Kwa Upande wake mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo aliahidi kuwa mkoa wa Arusha utatoa ushirikiano katika kuhakikisha kuwa unaondoa vikwazo kwa wakandarasi ili kuharakisha zoezi Hilo la ujenzi wa Makao makuu ya nchi za umoja wa Posta Afrika wa ghorofa 16.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/35xWy5E
via

Post a Comment

0 Comments