Ticker

10/recent/ticker-posts

SHAMBULIO LA UGAIDI LAUA WALIMU WATATU NCHINI KENYA

Na Ropota,Michuzi Globu ya jamii-Kimataifa

WALIMU watatu nchini Kenya wameripotiwa kuuawa baada ya kundi la watu wanaoshukiwa ni wanamgambo wa Al Shabab kuvamia Mji wa Garisa kaskazini mwa Kenya katika mpaka wa Kenya na Somalia.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirika la Habari la Uingereza(BBC) limesema leo Januari 13 mwaka huu wa 2020 kuwa walimu watatu ambao si wa eneo hilo walipigwa risasi hadi kufa, kituo cha polisi kikichomwa moto pamoja na mfumo wa mawasiliano kuharibiwa katika eneo la Kamuthe mapema leo asubihi.

Pia imeelezwa washambuliaji hao wameharibu mawasiliano kabla ya kutoroka.Hata hivyo maofisa wa Polisi wameanza kufuatilia wavamizi hao huku ripoti za kiusalama zikionoesha kuwa wavamizi wameweka vilipuzi chini ya ardhi katika barabara ya eneo hilo.

BBS imesema kuwa Kenya imekuwa katika hali ya tahadhari baada ya kupata taarifa za kijasusi kwamba kundi la Al Shabab linapanga kufanya mashambulio zaidi. Wiki iliyopita, Uingereza imetoa onyo kwa raia wake wanaotaka kusafiri nchini humo dhidi ya kutembelea kaunti ya Garissa na katika eneo la ndani ya kilomita 60 katika mpaka wa Kenya na Somalia.

Hilo ni shambulizi ya 11 kutekelezwa na kundi la Al Shabab nchini Kenya katika kipindi cha wiki sita.Mashambulizi manne yakitekelezwa Garissa, matatu Wajir, ,mawili eneo la Mandera na mawili mengine Lamu.


CHANZO -BBC


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/35PBtUh
via

Post a Comment

0 Comments