DOWNLOAD APP YETU HAPA

PETE ZA NDOA ZILIANZIA HAPA

  Masama Blog      
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

HISTORIA kuhusiana na pete ya ndoa ilianza miaka 3000 iliyopita huko Misri ambapo wapenzi walikuwa wakibadilishana Pete zenye madini ya thamani na zaidi waliamini kupeana Pete ni ishara ya kujizatiti katika mapenzi yao, walibadilishana Pete hizo wakiamini kuwa wanaweka nadhiri ambazo haziwezi kufa na mapenzi  hayawezi kukoma kwa kuwa duara ya pete hizo hauna mwanzo wala mwisho.

Huko Roma bwana harusi ndiye aliyekuwa anatoa pete ya ndoa ambayo ilikuwa ya chuma na kwa kiasi inafanana na pete za wakati huu ambazo zimewekwa nakshi na kuvutia na waliamini kuwa pete hizo huashiria uimara na kudumu, na imeelezwa kuwa Roma (wakatoliki) ndio walikuwa watu wa kwanza kuvishana Pete za ndoa, Waroma na Wagiriki huvishana Pete katika kidole cha nne cha mkono wa kushoto kwa kuamini kuwa kidole kina mshipa (vena amoris)uliofahamika kuwa ni mshipa wa mapenzi.

Nadharia nyingine ambayo imejiegemeza katika ndoa za kikristo ambapo padri huanzisha sala ambapo mume/ mke huelekeza Pete kuanzia kidole gumba, kidole cha shahada, kidole cha kati na kumaliza kwa kusema "kwa jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, na kumvisha pete hiyo na kumaliza kwa kusema Amina" tendo hilo humaanisha muungano kwa watu hao wawili.

Pete za ndoa huvaliwa mkono wa kushoto kwa jamii nyingi ila katika nchi za Ulaya Pete hizo huvaliwa katika  mkono wa kulia na sababu ya watu wengi kuvaa pete hizo mkono wa kulia ni kuepuka kuharibika hasa kwa wale wanaofanya shughuli zao kwa kutumia mkono wa kulia (right handed.)

Pete za ndoa katika wakati huu kwa tamaduni nyingi wanawake ndio huvaa pete za ndoa, hii pia ipo katika nchi za Ulaya ambapo katika kipindi cha vita ya pili wanajeshi na watoa huduma walikuwa wakivaa Pete zao ikiwa ni ishara ya kuweka maagano yao pamoja na njia ya kuwakumbuka wake zao hiyo ikaendelea  katika wakati wa Vita huko Korea na baadaye kuonea ulimwenguni pote ambapo aina mbalimbali za Pete za dhahabu na almasi zimeshika kasi.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2QH8AUL
via
logoblog

Thanks for reading PETE ZA NDOA ZILIANZIA HAPA

Previous
« Prev Post