HAPPY BIRTHDAY TO YOU GENERAL (Rtd) DAVID MUSUGURI....HOW OLD ARE YOU NOW....

  Masama Blog      
Mkuu wa Majeshi mstaafu Jenerali David Musuguri maarufu kama Jenerali ‘Chakaza’ au Mtukula, leo amesherehekea miaka 100 ya kuzaliwa kwake kwenye hafla iliyofanyika nyumbani kwake kijiji cha Butiama mkoani Mara kwa ibada maalum iliyongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Musoma, Michael Msonganzila. 
Pamoja na ibada hio,  maadhimisho hayo pia yamehusisha shughuli na sherehe za kifamilia, ikiwa ni pamoja na kukata keki na kuimbiwa "Happy Birthday to you".
Ibada ya shukrani inayofanyika nyumbani kwa mkuu huyo wa jeshi mstaafu imehudhuriwa na viongozi kadhaa wakiongozwa na Mbunge wa Musoma vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo. 
 Pamoja na kupanda ngazi mbalimbali za kijeshi, Jenerali Msuguri alikuwa Mkuu wa Majeshi kati ya mwaka 1980 hadi 1988. Katika moja ya mahojiano yake, aliwahi kusema alichukizwa na unyama ambao Idd Amin alikuwa anaufanya na angetokea akamkamata angemchinja. 
 Wakati wa vita ya Kagera, aliongoza vikosi vya Tanzania kumpiga aliyekuwa Rais wa Uganda, Idd Amin Dada, mwaka 1979, baada ya nduli huyo ambaye sasa ni alivuka mpaka na kuuvamia mkoa wa Kagera, Novemba 1978, hali ambayo Rais wa wakati huo, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere hakukubaliana nao na kutangaza kumpiga na kumwondoa. 
 Katika uvamizi huo, Amin alishusha bendera ya Tanzania na kupandisha bendera ya Uganda huku Watanzania ambao hawakuwa na hatia, wakubwa kwa wadogo, waliuawa na wengine kupata vilema vya kudumu, hali ambayo ilimuudhi Mwalimu Nyerere aliyetangaza vita.
Jenerali Musuguri  ndiye aliyeongoza Majeshi yaliyokomboa ardhi ya Tanzania na kumfurusha Iddi Amini hadi Kampala ambako alitoroka na kwenda kuishi uhamishoni Uarabuni.
Mkuu wa Majeshi mstaafu Jenerali David Musuguri maarufu kama Jenerali ‘Chakaza’ au Mtukula akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Adam Kighoma Malimja wakati wa kusherehekesa miaka 100 ya kuzaliwa kwake kwenye hafla iliyofanyika nyumbani kwake kijiji cha Butiama 
Mkuu wa Majeshi mstaafu Jenerali David Musuguri maarufu kama Jenerali ‘Chakaza’ au Mtukula akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Adam Kighoma Malima wakati wa kusherehekesa miaka 100 ya kuzaliwa kwake kwenye hafla iliyofanyika nyumbani kwake kijiji cha Butiama 

Mkuu wa Majeshi mstaafu Jenerali David Musuguri maarufu kama Jenerali ‘Chakaza’ au Mtukula akilishwa keki na Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Adam Kighoma Malima wakati wa kusherehekesa miaka 100 ya kuzaliwa kwake kwenye hafla iliyofanyika nyumbani kwake kijiji cha Butiama 
Mkuu wa Majeshi mstaafu Jenerali David Musuguri maarufu kama Jenerali ‘Chakaza’ au Mtukula akimlisha keki Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi  Mhe. Angelina Mabula  huku Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Adam Kighoma Malima akishuhudia wakati wa kusherehekesa miaka 100 ya kuzaliwa kwake kwenye hafla iliyofanyika nyumbani kwake kijiji cha Butiama from MICHUZI BLOG https://ift.tt/36mX3k0
via
logoblog

Thanks for reading HAPPY BIRTHDAY TO YOU GENERAL (Rtd) DAVID MUSUGURI....HOW OLD ARE YOU NOW....

Previous
« Prev Post