Ticker

10/recent/ticker-posts

UYUI KULIMA HEKTA 5,000 ZA PAMBA MSIMU HUU


WAKAZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Tabora(Uyui) wanatarajia kulima hekta 5,000 za zao la pamba katika msimu wa kilimo unaoendelea mkoani Tabora.

Kauli hiyo imetolewa juzi na Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya wakati akitoa taarifa ya kilimo cha zao hilo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora alipotembelea Wilaya hiyo kuhamasisha shughuli za kilimo.
Alisema kutokana na makadirio hayo wanatarajia kuzalisha tani 3,500 za zao hilo katika mavuno yajayo.

Msuya alisema jumla ya vyama msingi nane vimeshapokea mbegu na ugawaji kwa wakulima mbalimbali unaendelea.Mkuu huyo wa Wilaya alisema katika msimu uliopita walilenga kulima hekta 4,000 lakini walifanikiwa kulima hekta 1,700 na kuwafanikiwa kuzalisha kilo milioni 1.2.

Alisema katika kilo hizo wakulima walipwa shilingi milioni 1.5 ambapo wakulima wameshalipwa na Kampuni ya KCCL na KOM.Aidha alisema hadi hivi sasa Vyama vya Msingi vinadaiwa shilingi milioni 53.4 ikiwa ni gharama za mbegu na pembejeo.

Msuya alisema wamewaagiza Watendaji wa Vijiji kushirikiana na Askari wa Akiba kuhakikisha wanawabaini wale wote ambao wamechukua pembejeo na hawakulima na wale waliotorosha pamba yao ili waweze kulipa madeni yao. 

Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri aliwaagiza viongozi mbalimbali wa kuanzia ngazi ya Kijiji hadi Kata kulima kitaalamu ekari tatu za pamba ili kuwahamasisha wananchi wengi kushiriki katika kilimo hicho.

Alisema hatua hiyo itaisaidia Halmashauri yao kupata ushuru mwingi unaotokana na mauzo ya pamba ikiwa ni sehemu ya kuongeza mapato yake ya ndani



from MICHUZI BLOG https://ift.tt/35W8dMk
via

Post a Comment

0 Comments