Ticker

10/recent/ticker-posts

Taliss-IST yatwaa ubingwa wa U-12 kuogelea Taifa


 Waogeleaji chipukizi wakichumpa wakati wa mashindano yaliyofanyika kwenye bwawa la kisasa la Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST)- Masaki.
Waogeleaji chipukizi wakiwa katika pozi baada ya kuzawadiwa medali zao kwa kushinda ‘relay’
Mama na Mwana! Meneja wa timu ya Taliss-IST, Hadija Shebe akisheherekea na mwanaye, Nawal Shebe wakati wa mashindano ya kuogelea ya yoso chini ya miaka 12.
Waogeleaji chipukizi wakiwa katikan pozi baada ya kuzwadiwa medali zao.
……………
Na Mwandishi wetu
Dar es Salaam. Klabu ya kuogelea ya Taliss-IST imefanikiwa kutwaa ubingwa wa taifa kwa waogeleaji wenye umri chini ya miaka 12.
klabu hiyo imezipiku klabu tisa baada ya kupata  jumla ya pointi 1,736 katika mashindano yaliyofanyika kwenye bwawa la kuogelea la kisasa la Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST)- Masaki.
Waogeleaji wavulana wa klabu hiyo wamechangia pointi nyingi kwa timu yao baada ya kukusanya 948 huku upande wa wanawake  wakipata pointi 788.
Meneja wa Taliss-IST, Hadija Shebe  aliwapongeza wachezaji wake kwa kuendeleza ushindi katika mchezo huo na kuiletea sifa klabu yao.
“Siri kubwa ya  ushindi kwa klabu yetu ni ushirikiano baina ya wazazi, makocha na moyo wa kujituma kwa waogeleaji, nawapongeza wachezaji kwa kufanya vyema,” alisema Hadija.
Klabu inayokuja kwa kasi ya Bluefins imemaliza nafasi ya pili kwa kukusanya pointi 1,521 ambapo kwa upande wa wanawake, klabu hiyo imekuwa ya kwanza kwa kupata pointi 798 na pointi 723 zilikusanywa na waogeleaji wanaume.
Nafasi ya tatu imechukuliwa na klabu ya Dar Swim Club (DSC) kwa kupata pointi 779 ambapo kwa upande wa wanawake  klabu hiyo ilikusanya pointi 385 na wanaume walikusanya pointi 394.
Klabu mpya kabisa katika mchezo huo, FK Blue Marlins imeshika nafasi ya nne kwa kupata pointi 778 ambapo kwa upande wa wanawake, klabu hiyo ilipata jumla ya pointi 597 na wanaume pointi 181.
 Nafasi ya tano ilichukuliwa na klabu ya Uwcea ya Moshi kwa kupata pointi  294 huku Champion Rise ikishika nafasi ya sita kwa pointi 220, Mis Pirahnas ya Morogoro (150 pointi, nafasi ya saba), Wahoo Zanzibar (106 pointi, nafasi ya nane), Mwanza (98 pointi, nafasi ya tisa na nafasi ya 10 ilishikwa na klabu ya Arusha iliyopata pointi tano.
Mashindano hayo yalishirikisha jumla ya waogeleaji zaidi ya 150 ambao walishindana katika staili mbalimbali ambazo ni freestyle, butterfly, backstroke, Breaststroke na Individual Medley (IM).
Waogeleaji hao pia walishinda katika ‘relay’ ambayo ilikuwa ya kusisimua na ushidano mkubwa.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2P0GVhT
via

Post a Comment

0 Comments