Ticker

10/recent/ticker-posts

KAMPUNI YA URSINO YAFADHILI WATOTO WALIOFANYA VIZURI KWENYE MASOMO KUTEMBELEA HIFADHI YA SAANANE










walimu wakipata chakula baada ya kutembelea hifadhi jana.

Mkurugenzi wa kampuni ya URSINO Ltd Mhandisi Mnandi Mrutu Mnandi wa nane kutoka kulia akiwa katika picha ya pmoja na walimu na wanafunzi wa shule ya Kilimani sekondari baada ya kumaliza kutembelea hifadhi ya Saanane jana.wa saba kutoka kulia ni Mkuu wa shule hiyo Gerana Majaliwa.

Wanafunzi wakipata chakula cha mchana baada ya kumaliza ziara ya kutembelea hifadhi ya Saanane jana.

********************************

NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA

MKURUGENZI wa Kampuni ya URSINO Ltd, Mhandisi Mnandi Mrutu amesema mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano ndani ya miaka minne hayana mfano, yanawavutia wananchi wengi kutokana na kutekeleza ahadi na miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo elimu bure kwa kasi ya ajabu.

Alisema hayo jana wakati wa ziara ya kutembelea Hifadhi ya Saanane aliyowaandalia wanafunzi 30 wa kidato cha kwanza na cha pili wa shule ya sekondari Kilimani iliyopo Manispaa ya Ilemela waliofanya vyema kwa kupata daraja la kwanza kwenye masomo yao.

Mhandisi Mrutu lisema Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais John Magufuli ni ya kupigia mfano kwenye maendeleo yaliyopatikana nchini ikiwa ni pamoja na elimu bure na hivyo anastahili kuungwa mkono na kila Mtanzania.

Alisema serikali imefanya kwa kasi mambo makubwa ya maendeleo ya ajabu na kuhakikisha watoto wa wananchi wanyonge wanapata elimu bure bila malipo waweze kutimiza ndoto zao kimaisha na katika kuunga mkono juhudi hizo aliamua kufadhili ziara ya utalii kimasomo ili kuwahamasisha watoto kujifunza kwa vitendo na kuwa wazalendo wa kutangaza hifadhi zetu.

Alidai kuwa nidhamu,uwezo na ufaulu wa wanafunzi wa shule hiyo ya umma ulimvutia wakati akitekeleza ahadi ya Rais John Magufuli ya kumtua mwanamke ndoo ya maji kichwani,kwa kutumia kipato chake kidogo aliahidi kuwa motisha ya kutembelea Hifadhi ya Saanane ili kuwajenga kuwa wazalendo na kuondokana na ubinafsi.

“Nidhamu ya watoto wa shule hii ya kata ilinivutia nikaahidi kuwalipia ada wananfuzi 30 waliopata daraja la kwanza kwenye masomo yao wakatalii kwenye hifadhi ya Saanane ambayo ni urithi wetu ili kuunga juhudi za Jemedari wa vita na mpenda maendeleo, kwani maendeleo ya kijamii na kielimu yanakuja kwa kasi.Rais pia anatupenda tumuunge mkono kwa kutembelea hifadhi kujenga uchumi na maendeleo,”alisema Mhandisi Mnandi.

Alisema Rais, Dk. Magufuli, mambo anayoyafanya ni kwa maslahi ya nchi , jambo la pekee ambalo ni urithi wa kila mtoto ni kubeba kwake elimu bure ambayo imeunganisha Watanzania,hivyo akishirikiana na mlezi wa shule ya Kilimani Salum Kalli ambaye ni Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, walitumia fursa kipato chao kidogo kuwezesha ziara hiyo watoto waliofanya vizuri kwenye masomo na kupata daraja la kwanza, kujifunza utalii kwa vitendo badala ya nadharia.

“Tudumishe utalii wetu wa ndani tusisubiri wageni wanatoka nje wao kuja kutembelea, wakati sisi watanzania wenyewe,tuko hapa tunatakiwa kufurahia fursa hizi, kwanza ukiangalia bei ni affordable kwa watanzania serikali imetoa upendeleo kwa dhati kabisa kuwapendelea watanzania, maana inawapenda wananchi wake lakini pia tunawapenda na wageni.

Alisema Tanzania hatubaguani kwa sababu tumerithishwa na Mwalimu Julius Nyerere,kwamba Watanzania hatuulizani wewe kabila gani na tunatakiwa kufurahia sana hasa wana Mwanza, Mheshimiwa Rais kwa namna anatekeleza ahadi.

“Ona hata juzi Kilimanjaro kapeleka treni huwa inakwenda inabeba ndugu zetu wale,ndege zinazonunuliwa,majengo yanajengwa,vivuko vinajengwa, sasa na mimi nimeifanyia nini serikali ndiyo sasa tunakuwa wazalendo vitu kama hivi tunawapa hamasa vijana wetu na wao wawe wajifunze kuwa wazalendo tuondoe sasa ile dhana ya umimi, ubinafsi tushrikiane pamoja ili watoto pindi watakapokuwa waweze kuhadithia hizi hifadhi zetu wazitangaze wawe mabalozi wazuri wa Rais ,”alisema Mhandisi Mnandi na kuongeza;”

“Usiseme tu kuna mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya hapana hao wapo lakini na wewe mwananchi wa kawaida umeifanyia nini serikali yako, unafanya nini kuwa motivat hawa wanafunzi, unafanya nini kuzi motivat hizi shule zetu za serikali ambazo zinamejengwa na zitakazojendelea kujengwa.’

Aliongeza kuwa kipekee anamshukuru Dk.Magufuli na Mkuu wa mkoa wetu wa Mwanza, kwa jinsi wanavyoendesha nchi na mkoa, anamuombea Rais kwa Mungu ambariki, ampe maisha marefu amuongoze katika kazi zake, ni kiongozi ambaye yeye hajapata kuona, japo anawahesimu viongozi waliopita walifanya yao kwa uwezo wao ulipofikia lakini inayokuja sasa ni tsunami.

Mkuu wa shule hiyo ya Kilimani,Gerana Majaliwa ,alisema ziara hiyo ni moja ya malengo waliyojiwekea ya kuwapa motisha wanafunzi wanaofanya vizuri kwenye masomo kupiti utalii huo wa ndani ushindani na ufaulu utaongezeka.

“Wanafunzi hawa kwenye hifadhi hii ya Saanane wamejifunza kwa vitendo baada ya kuwaona wanyama, mijusi na ndege wa aina mbalimbali na kupata ufahamu nini maana ya utalii ikizingatiwa Mada ya Utalii inafundishwa kidato cha pili, watahamasika wenyewe pamoja na jamii kutembelea hifadhi badala ya kuwachia wageni kutoka nje,”alisema Majaliwa.

Naye Dada Mkuu wa Shule hiyo Dorin Stumai alisema wamejifunza mambo mengi ya kijamii na kielimu kuhusu matunzo,vyakula na tabia za wanyama wakiwemo simba,mamba, ndege tausi tumbili na viumbe vingine hifadhini hapo ingawa awali utaii waliusoma kwenye Jiografia .

Aliihasa jamii na Watanzania kufanya utalii wa ndani kwa kutumia urithi huo kujenga uchumi wetu kwa maslahi yetu na kuacha kusubiri wageni ingawa wanachangia kuongeza pato la taifa ambapo aliwashukuru Mkurugenzi wa kampuni ya URSINO Ltd (Mnandi Mrutu) na mlezi wa shule hiyo, Katibu wa CCM wa Mkoa wa Mwanza (Salum Kalli) kwa kuwezesha ziara hiyo.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2Qj8fY5
via

Post a Comment

0 Comments