DIT YAANDAA MAONESHO MAALUM YA TEKNOLOJIA MBALIMBALI ZA TEHAMA

  Masama Blog      

KATIKA shamra shamra za maafali ya 13 ya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) ambayo yatafanyika Disemba 12 mwaka huu, wamendaa maonyesho maalumu ya teknolojia mbalimbali za TEHAMA ambapo pamoja na mambo mengine huduma mbalimbali kwa wananchi zitatolewa ikiwa ni pamoja na kutengenezewa simu pamoja na kompyuta zao.

Mhadhili Msaidizi wa DIT, Daudi Mboma anasema Taasisi hiyo imeandaa maonyesho maalum ya Tehama ambayo yapo chini ya mradi wa Escrip unaofadhiliwa na Benki ya Dunia.

Amesema mradi huo utaanzishwa katika Kampasi ya Dar es Salaam ambapo wataanzisha kituo cha ICT ambayo itakuwa ya kikanda itakayojikita hasa katika usalama wa mitandao.

"Tumeandaa baadhi za wabunifu wanafunzi hapa kwenye Taasisi na wengine ambao wameanzia hapa kwetu na sasa wanajitegemea wamefanikiwa kuanzisha kampuni zao, watakua hapa kuanzia leo hadi siku ya mahafali wakitoa huduma ya kutengeneza kompyuta na simu bure," anasema Mboma.

Karuma Nicholas ni Mwanafunzi aliyesoma katika Taasisi hiyo na ni mmiliki wa kampuni ya Testlimit, anasema elimu inayotolewa DIT ni ya kipekee kwani wanafundisha zaidi kwa vitendo Jambo lililomuwezesha kufanya kazi nyingi za TEHAMA.

Wananchi wanaalikwa katika viwanja vya Taasisi hiyo kutembelea maonesho hayo kujifunza pamoja na kupata huduma bure ya kutengenezewa simu pamoja na komputa zao.

from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2EcyWYJ
via
logoblog

Thanks for reading DIT YAANDAA MAONESHO MAALUM YA TEKNOLOJIA MBALIMBALI ZA TEHAMA

Previous
« Prev Post