DIRA YA SERIKALI YAZIDI KUWAVUTIA WAWEKEZAJI NCHINI

  Masama Blog      
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
DIRA ya Serikali ya awamu ya tano ambayo imejikita katika ujenzi wa viwanda imezidi kuwavutia wawekezaji wengi zaidi wenye uhitaji wa kuwekeza na kutengeneza masoko zaidi nchini, ambapo leo Desemba 05 kampuni ya JK White cement (Afrika) Limited ambayo ni sehemu ya kampuni ya JK ya nchini India imetangaza rasmi kuungana kibiashara na kampuni ya uzalishaji wa rangi ya Goldstar Paints ya Tanzania ili kuingiza sokoni bidhaa mpya ya JK Wall Putty bidhaa ambayo ni poda laini itokanayo na saruji nyeupe yenye kutoa mwonekano mzuri kwa kuta na dari ambayo itaenda sambamba na mazingira.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa JK cement Amit Kothari amesema, ushirikiano huo wa kibiashara umelenga kukata kiu ya wananchi kwa kutoa bidhaa bora yenye kuendana na mazingira.

"JK cement ni moja kati ya wazalishaji bora wa cement na tumepata  washirika makini ambao tutaziba ombwe lililopo pamoja na kutoa ajira, na kubwa zaidi ni kufungua ofisi na kupandisha bendera Tanzania kwa mara ya kwanza katika ukanda wa Afrika na dunia, na hiyo ni kutokana na ushirikiano mzuri tunaooneshwa na Serikali ya Tanzania" ameeleza Kothari.

Amesema kuwa wanajivunia kuwa sehemu ya watanzania na kueleza kuwa kampuni hiyo isiitwe ya wahindi bali watanzania kwa kuwa Goldstar Paint wamekuwa kwenye safari na dhamira ya kutoa bidhaa zenye ubora zenye kukidhi mahitaji ya watanzania kupitia bidhaa zao.

Kwa upande wake  Mkurugenzi Mtendaji wa Goldstar Srinivasan amesema kuwa  kampuni hiyo imekuwa mstari wa mbele  hasa katika masoko kwa Kuhakikisha kwamba inaleta bidhaa zenye viwango stahiki na kwa sasa wameongeza bidhaa nyingine kwenye soko jambo ambalo wanaamini litaleta mabadiliko na mapinduzi katika kuwahudumia wateja.

Amesema kuwa, JK ikiwa moja kati ya kampuni kubwa za uzalishaji wa saruji nyeupe duniani na mzalishaji mkuu wa bidhaa ya Wall Putty nchini India  wataendelea kuwahudumia watanzania kwa kuwapa bidhaa bora zaidi ambazo zinaendana na mazingira.

Kampuni ya JK cement yenye makazi yake Fujairah (UAE) wamekuwa wadau kwa nchi za Afrika na katika kujipapanua zaidi  wamejiegemeza zaidi katika kukuza soko lake Tanzania kupitia muungano huo wa kibiashara na kampuni ya Goldstar iliyoanzishwa mwaka 1988 ambao wamekuwa maarufu zaidi kupitia rangi ya Goldstar ambayo hupatikana kote nchini na ilichaguliwa miongoni mwa makampuni 50 bora zaidi nchini na TBS na TPSF mwaka 2017.
Mkurugenzi Mkuu wa JK cement Amit Kothari akizungumza wakati wa hafla ya makubaliano ya kibiashara yaliyofanyika kati ya kampuni ya JK cement na kampuni ya Goldstar Paints ambapo ameeleza kufurahishwa na Serikali katika suala zima uwekezaji, leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Goldstar Paints K. Srinivasan akizungumza wakati wa hafla ya makubaliano ya kibiashara yaliyofanyika kati ya kampuni ya JK cement na kampuni ya Goldstar Paints ambapo amesema kuwa wataendelea kutoa huduma kwa Bora kwa watanzania, leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Goldstar Paints K.Srinivasan (kushoto) akipeana mkono na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya JK Cement Amit Kothari kama ishara ya kupongezana na kufanya kazi pamoja, leo jijini Dar es Salaam.
Viongozi wa kampuni hizo  na wadau wa 5mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/33S9jqL
via
logoblog

Thanks for reading DIRA YA SERIKALI YAZIDI KUWAVUTIA WAWEKEZAJI NCHINI

Previous
« Prev Post