BEN POL AWAPA ZAWADI YA 'SIKUKUU' MASHABIKI ZAKE

  Masama Blog      


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Mkali wa R n B nchini Benard Paul 'Ben Pol' ametoa zawadi ya Krismasi kwa mashabiki wake baada ya kuachia kibao kipya kinachoitwa Sikukuu.

Ben Pol ameachia nyimbi hiyo mapema wiki hii ikiwa ni maalumu kwa mashabiki wake na ukiwa ni wimbo maalumu wa sikukuu.

Kwa upande Ben Pol amesema, ameamua kuutoa wimbo huu ukiwa ni kama zawadi ya sikukuu kwa mashabiki zake ili uweze kuwaburudisha katika kipindi chote cha Sikukuu za Krismasi na mwaka mpya.

Amesema, wimbo huo ameutengeneza kwa Producer Tiddy Hotter Kwenye studio za One Love Records huku upande wa Video akisimama mkongwe Adam Juma.

"Wimbo huu ww nimeupa jina jina la sikukuu kwakuwa ni zawadi kwa mashabiki zangu, na jana rasmi niliweza kuuachia Audio na Video, zote kwa pamoja,"amesema

Aidha, Ben Pol amesema anaamini mashabiki wake wataupokea vyema wimbo wake huu mpya alioutoa mahususi kwa ajili yao.

Msanii huyo, anayeimba miondoko ya R n B amekuwa katika muendelezo mzuri wa Kisanii baada ya hivi karibuni aliweza kushirikishwa wimbo wa Nipokeeni ulioimbwa ba Chid Benz, huku kwa upande wake nyimbo zake za Wapo na Sana bado zikiendelea kufanya vizuri.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2EJqIaN
via
logoblog

Thanks for reading BEN POL AWAPA ZAWADI YA 'SIKUKUU' MASHABIKI ZAKE

Previous
« Prev Post