Ticker

10/recent/ticker-posts

WAZIRI HASUNGA APIGILIA MSUMARI, SERIKALI HAITOPANGA BEI ELEKEZI YA MAHINDI NA MCHELE

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akichimba mashimo kwa ajili ya kupanda mahindi wakati akizindua msimu wa kilimo Kitaifa mwaka 2019/2020 leo tarehe 22 Novemba 2019 katika eneo la Vwawa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa pamoja na wakulima wakisafisha shamba kwa ajili ya kupanda mahindi wakati akizindua msimu wa kilimo Kitaifa mwaka 2019/2020 leo tarehe 22 Novemba 2019 katika eneo la Vwawa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa shambani wakati akizindua msimu wa kilimo Kitaifa mwaka 2019/2020 leo tarehe 22 Novemba 2019 katika eneo la Vwawa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiondoka shambani akiwa pamoja na wakulima mara baada ya kumaliza kazi ya kupanda mahindi wakati akizindua msimu wa kilimo Kitaifa mwaka 2019/2020 leo tarehe 22 Novemba 2019 katika eneo la Vwawa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe.



Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songwe

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) leo tarehe 22 Novemba 2019 amezindua msimu wa kilimo Kitaifa mwaka 2019/2020 ambapo amewataka wakulima kote nchini kulima mazao ya chakula na biashara kwani serikali inaendelea kuimarisha masoko ya mazao ndani na nje ya nchi.

Katika uzinduzi huo wa msimu wa kilimo uliofanyika katika eneo la Vwawa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe amewahakikishia wakulima kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli imeanzisha kitengo cha masoko chini ya wizara ya Kilimo ambacho moja ya kipimo chake kiutendaji ni kutafuta masoko ya mazao ya wakulima ndani na nje ya nchi.

Alisema serikali imeweka msisitizo katika kuimarisha mazao mbalimbali ya chakula, biashara pamoja na mazao ya mbogamboga na matunda hivyo wakulima hawapaswi kuwa na wasiwasi na masoko ya mazao yao kwani yataendelea kuimarika maradufu.

Mhe Hasunga ameitaka Mamlaka ya udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) kuhakikisha kuwa inasimamia utekelezaji wa maagizo ya serikali ya kuhakikisha kuwa wafanyabiashara wanauza mbolea kwa bei elekezi ili kuwanufaisha wakulima kwani mbolea ni miongoni mwa Pembejeo muhimu kwa ajili ya kuhakikisha kuwa wakulima wanalima mazao yenye tija.

Alisema kuwa mfanyabiashara yeyote atakayebainika kuuza mbolea zaidi ya bei elekezi anapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufutiwa leseni ya kufanya biashara hiyo.

Kuhusu Mbegu za mazao, Mhe Hasunga ameitaka Taasisi ya Udhibiti wa mbegu nchini (TOSCI) kuhakikisha kuwa mbegu zinazopelekwa kwa wakulima nchini zinakuwa katika ubora unaostahili huku akiagiza wauzaji wa mbegu feki kuchukuliwa hatua.

“Vilevile naagiza Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) kuhakikisha kuwa wanazalisha mbegu za kutosha na kuzifikisha kwa wakulima kwa wakati ili katika msimu wa kilimo wa mwaka 2019/2020 kuwa na uzalishaji mkubwa na tija kwa wakulima” Alisema.Kwa upande wa Viuatilifu, Waziri Hasunga ameiagiza Taasisi ya Utafiti na Udhibiti wa Viuatilifu ukanda wa Kitropiki (TPRI) kuhakikisha wanafanya ukaguzi nchi nzima ili kubaini na kuondoa viuatilifu feki vyote sokoni.

Ameongeza kuwa TFRA inapaswa kutoa elimu ya kutosha kwa wakulima kote nchini kuhusu matumizi sahihi ya Viuatilifu ili kuondoa dhana ya wakulima kuwa na malalamiko mengi kuhusu viuatilifu.

Aidha, Mhe Hasunga amesisitiza kuwa serikali inayoongozwa na Dkt Magufuli haitawapangia bei ya mazao yao wakulima hususani mazao makuu ya chakula na biashara kwani wakulima wanapokuwa wanalima mazao yao hakuna watu wanaowasaidia hivyo wakati wa kuuza pia wanapaswa kuamua bei kulingana na soko.

Mhe Hasunga pia amewataka wakulima kujihusisha zaidi na kilimo kinachozingatia hifadhi ya udongo (Climate Smart Agriculture) kwa kuchimba mashimo na kupanda mbegu kuliko kilimo kinachoharibu udongo kilichozoeleka.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/34fvbgC
via

Post a Comment

0 Comments