Ticker

10/recent/ticker-posts

WANAHARAKATI WAWAASA WAGOMBEA WA UCHAGUZI SERIKALI ZA MTAA KUJITAFAKARI UPYA

 Mwanaharakati wa Mambo ya kijamii, Mackdeo Shilinde akizungumza jijini Dar es Salaam leo na kuviasa vyama vya siasa kutunza afya ya demokrasia hapa nchini.
Mwanaharakati wa Mambo ya kijamii, Mackdeo Shilinde akizungumza jijini Dar es Salaam leo na kuviasa vyama vya siasa kutunza afya ya demokrasia hapa nchini. Kulia ni Mwanaharakati kutoka ADO, Ally Mwinyi.
Baadhi ya Waandishi wa habari.

Na Avila Kakingo,Glou ya Jamii
WANAHARAKATI wa mambo ya kijamii wamewasa viongozi wa vyama vya upinzani nchini kujitafakari upyaa jinsi wagombea wao wa uchaguzi wa serikali za mtaa wanavyojitoa katika nafasi walizochaguliwa kugombea   uchaguzi wa serikali za mtaa unaotarajia kufanyika Novemba 24,2019 nchini kote.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mwanaharakati wa Mambo ya kijamii, Mackdeo Shilinde, amesema kuwa mambo yanayotakiwa yafanyike na chama pamoja na wagombea yafanyike kwa haki na kwa amani kwani wananchi wapo tayari kuchagua kiongozi wanae mtaka.

"Viongozi wa vyama vya upinzani warudi tena wakatafakari na wagombea wao wakawashirikishe waseme je ni kweli wagombea wao hawataki kushiriki kwenye uchaguzi wa serikali za mtaa? lakini vilevile vyama vya upinzani wakafate taratibu wa katiba yao kwenye mambo yanayotakiwayafanyike yafanyike." Amesema Shilinde

Hata hivyo Mwanaharakati wa mambo ya kijamii kutoka taasisi isiyo ya kiserikali ya  Alliance for Development (ADO), Ally Mwinyi amesema kuwa wagombea wa vyama vya upinzani wanaojiondoa kugombea katika uchaguzi wa serikali za mtaa wanadhoofisha afya ya demokrasia nchini na kuwanyima wananchi demokrasia ya kuchagua kiongozi wanaye mtaka.

"Jambo hili la kujitoa kwenye uchaguzi wa serikali za mtaa si jambo zuri kwa afya ya Demokrasia na ni kuwanyima wananchi demokrasia ndani ya demokrasia"

Mwinyi amesema kuwa demokrasia ni kuwa tayari kufata zile hatua zote za uchaguzi kwa sababu zisipofatwa ni kuharibu kanuni na taratibu zilizowekwa kwaajili ya afya ya Demokrasia.

Hata hivyo Mwinyi amesema kuwa kitendo cha baadhi ya vyama vya siasa kutoa tamko kabla  ya majibu ya rufaa zao hayajatoka hii si picha nzuri kwani vyama hivyo kwani vinasigina demokrasia.

"Sisi kama wanaharakati tunachopenda kutoa rai yetu kwa vyama viheshimu demokrasia, vionyeshe kuwa wao ndio wa kwanza wa kuonyesha afya ya demokrasia".

Mwinyi amesema kuwa watanzania wanahitaji watu kwaajili ya kuwatetea pamoja na kuwaongoza na hakuna njia nyingine isipokuwa ni kufanya uchaguzi kwa kufata taratiu zilizowekwa.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2Kbxrxr
via

Post a Comment

0 Comments