Ticker

10/recent/ticker-posts

SERIKALI YAOMBWA KUKOMESHA MAUAJI NA UBAKAJI KWA KINAMAMA NA WATOTO WA KIKE .

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo (mwenye shati jekundu)akiteta jambo na diwani wa kata ya Olasiti,kushoto kwake ni Katibu Tawala wa mkoa huo Richard Kwitega,kulia kwake ni Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha Jonathan Shana.


Na.Vero Ignatus,Arusha.

Serikali ya mkoa wa Arusha imeombwa kukomesha vitendo vya mauaji na ubakaji katika kata hiyo vilivyoshamiri na kuwa tishio hasa kwa kinamama na watoto wa kike ambao wamekua wahanga wa matukio hayo ambayo yamekua yakijitokeza mara kwa mara

Akizungumza Diwani wa kata ya Olasiti Alex Martin katika ziara ya Mkuu wa Mkoa Mrisho Gambo aliyetembelea katika shule ya sekondari Mrisho Gambo ambapo alikagua ujenzi unaondelea na kuzungumza na wananchi ,Diwani huyo ameiomba serikali iweze kutumia vyombo vyake vya ulinzi kukomesha mauaji hayo.

Diwani huyo ameiomba serikali kujenga kituo kidogo cha polisi kitakachosaidia kuimarisha ulinzi na usalama wa raia kwani eneo hilo halina kituo cha polisi hivyo suala la ulinzi wa watu linakua gumu.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa Mrisho Mashaka Gambo akijibu Diwani huyo,ameitaka kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya na Mkoa kufika katika kata olasiti na kushughulikia tatizo la mauwaji kwa kina mama na watoto pamoja na viteno vya ubakaji ili kutokomeza vitendo hivyo na kurejesha hali ya usalama.

Mhe.Gambo anetoa agizo hilo katika ziara yake ya kikazi ya siku mbili ya ukaguzi wa maendeleo ya jiji la Arusha katika ukaguzi wa mradi wa elimu shule ya sekondari Burka iliyopo kata ya olasiti Na kupokea jumla ya madawati na viti zaidi ya 170 kutoka katika taasisi ya kifedha ya NMB Kanda ya kasikazini pamoja na mifuko Hamsini ya simenti kwajili ya ujenzi wa shule hiyo kutoka kanisa la EAGT mkoani Arusha.

Aidha amesema kuwa tukio la kinamama na watoto kuuliwa na kubakwa linasikitisha kwani serikali haiwezi kuvumilia kuona matukio hayo yakiendelea huku kukiwa na watu wanaokisiwa kufanya matukio hayo ambapo ameitaka kamati ya ulinzi na usalama mkoa huo kufanyia uchanguzi na kushuhurikia swala hilo.

Kwa upande wao Wananchi Zainab Kasanga na Joseph Simon wa kata hiyo wamekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kushukuru ujio wa Mkuu wa Mkoa ambao unaweza kuwa suluhu kwa changamoto hiyo ya matukio ya ubakaji na mauaji ambao yamekua yakitikisa kata hiyo


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2qnNO38
via

Post a Comment

0 Comments