Ticker

10/recent/ticker-posts

MRADI WA MAJI WA KISARAWE KUANZA KUTOA MAJI MWEZI UJAO

Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akimsikiliza Mkurugenzi wa Uwekezaji na Miradi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Mhandisi Ramadhani Mtindasi katika kituo cha kusukumia maji Kibamba, wilayani Ubungo.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) pamoja na Mkuu wa Wilaya za Ubungo, Kisare Makori (kulia) na Mkuu Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo (kushoto) katika ziara ya kufuatilia utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Kisarawe, katika Kata ya Kibamba, wilayani Ubungo.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiwa na mkandarasi alipotaka maelezo kuhusu utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa kwake jana ya kukamilisha utaratibu wa malipo na kazi ya kuvuta umeme.
Tenki la maji la Kibamba lenye ujazo wa lita milioni kumi litakolotumika kuhifadhi maji yatakayo hudumia wakazi wa Kisarawe kupitia Mradi wa Maji wa Kisarawe.



Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiwa na Msimamizi wa Ujenzi wa Mradi wa Maji wa Kisarawe, Mhandisi Ishmaeli Kakwezi wakati akikagua tenki la maji la Kibamba lenye ujazo wa lita milioni 10.

Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiwa kwenye eneo palipo na maunganisho ya bomba la tenki la Kibamba na bomba linalopeleka maji katika Mji wa Kisarawe.
…………………….

Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) ametembelea na kukagua utekelezaji wa kazi ndogo zilizobaki katika ujenzi wa Mradi wa Maji wa Kisarawe katika Kata ya Kibamba, wilayani Ubungo.

Ziara imelenga kufuatilia utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa jana kwa mkandarasi kukamilisha utaratibu wa malipo na kazi ya kuvuta umeme ifanyike haraka ili mradi uanze kufanya kazi mwezi ujao.

Malipo ya Shilingi milioni nane kwa TANESCO yameshafanyika na kazi ya kufunga umeme huo itaanza mara moja tayari kwa kufanya majaribio ya kusukuma maji (pump test) wiki ijayo.

Katika ziara hiyo Naibu Waziri Aweso ameambatana na Wakuu wa Wilaya za Ubungo, Kisare Makori na Kisarawe, Jokate Mwegelo akiwasisitiza umoja na ushirikiano katika kufanikisha zoezi la utekelezaji wa mradi huo kwa maslahi mapana ya wananchi wa Kisarawe. 

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makori ametoa rai kwa viongozi na watendaji wa wilaya za Ubungo na Kisarawe kujitoa na kusimamia miradi ya maendeleo inayotumia fedha nyingi, hatua itakayosaidia juhudi za Serikali kuzaa matunda.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2ozE455
via

Post a Comment

0 Comments