Ticker

10/recent/ticker-posts

LONGIDO YAKAMATA WAHAMIAJI HARAMU KUTOKA SOMALIA,WAKUTWA NA NGAMIA 200

Na Woinde Shizza,Globu ya Jamii Arusha

MKUU wa Wilaya ya Longido Frank Mwaisumbe ameongoza operesheni ya kuwakamata waahamiaji haramu kotoka nchini Somalia wakiwa na ngamia 200 pamoja nyaraka mbalimbali kutoka nchi ya Kenya.

Akizungumza leo wilayani hapa mara baada ya kuwakamata baadhi ya wahamiaji hao haramu

kutoka nchini Somalia,Mkuu huyo wa Wilaya wamefanikiwa kuwakamata baada ya kupata taarifa kuwa katika mpaka wetu wa Namanga upande wa Magharibi ndani ya kata ya Kimkoa ambayo ina karibu kilometa 30 kutoka Mjini Namanga kuna watu wasiojulikana wameweka makazi(kempu).

Amesema baada ya kupata taarifa hizo walikwenda kufanya operesheni na kufanikiwa kuwakamata watu wawili wenye asili ya nchi ya Somalia na hakuwa na uwezo wa kuzungumza lugha ya Kiswahili huku wengine wao wakiwa wamekimbia

"Tulienda na Kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya pamoja na baadhi ya askari kutoka mkoani, katika eneo hilo tumefanikiwa kuwakamata wahamiaji hao haramu wawili.Wengine wamekimbia,"amesema Mkuu wa Wilaya Mwaisumbe

Amefafanua baada ya kuwakamata walifanikiwa kuwakuta na mifugo aina ya na ngamia zaidi ya 200 pamoja na nyaraka mbalimbali kutoka nchi ya jirani ya Kenya.

Amesema kuwa operesheni hiyo haitaishia hapo bali itaendelea kwa lengo la kuhakikisha watu wote ambao wameingia nchini bila utararibu na kuweka makazi ya kudumu wanachukuliwa hatua na kutoa rai kwa wananchi kutoa taarifa wanapoona kuna watu wameingia nchini kwetu.

Wakati huo huo Mwaisumbe amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo na kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa kwa ushirikiano ambao umefanikisha kukamatwa kwa watu hao pamoja na mifugo yao ya ngamia.Kwa upande wake Mkaguzi wa Uhamiaji ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha

Udhibiti na Usimamizi wa mipaka Mkosa wa Arusha Elisamia Mmari amesema kwa utaratibu wa uhamiaji watuhumiwa hawa watapelekwa katika ofisi za uhamiaji na watachukuliwa maelezo baada ya hapo watafikishwa katika vyombo vya sheria ili iwefundisho kwa watu wote wanaiongia nchini na kufanya shuhuli za bila kufata taratibu.

Mwisho


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2Ct9DAV
via

Post a Comment

0 Comments