Benki ya NBC yadhamini Gofu ya Mabalozi visiwani Zanzibar

  Masama Blog      

Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Damas Ndumbaro (kushoto), Mbunge wa Kenya, Kassim Sawa (kulia), na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi Maalum wa Benki ya NBC, Ashura Waziri (wa pili kulia), wakimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa mashindano ya kwanza ya gofu ya mabalozi, Eliah John yaliyodhaminiwa na Benki ya NBC kama moja ya shughuli za kuisapoti sekta ya michezo na utalii nchini. Mashindano hayo yalifanyika katika viwanja vya gofu vya Sea Cliff kisiwani Zanzibar jana.
Meneja wa NBC Tawi la Zanzibar, Ramadhani Lesso (kushoto) akipongezana na Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Damas Ndumbaro, huku mchezaji mwenzao Mbunge wa Kenya, Kassim Sawa akiwangalia wakati wa mashindano ya kwanza ya gofu ya Mabalozi yaliyofanyika katika viwanja vya gofu vya Sea Cliff kisiwani Zanzibar jana. Mashindano hayo yalidhaminiwa na Benki ya NBC kama moja ya shughuli za kusapoti sekta za michezo na utalii nchini.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Damas Ndumbaro (kulia) akimkabidhi zawadi mshindi wa pili wa mashindano ya kwanza ya gofu ya mabalozi, Issa Mohamed Chaap yaliyodhaminiwa na Benki ya NBC ikiwa ni sehemu ya shughuli za kusapoti sekta za michezo na utalii nchini. Mashindano hayo yamefanyika katika viwanja vya gofu vya Sea Cliff kisiwani Zanzibar jana.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Damas Ndumbaro (kushoto) akipokea zawadi ya kushiriki katika Mashindano ya kwanza ya gofu ya mabalozi kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Wateja Rejareja Maalum wa Benki ya NBC, Ashura Waziri yaliyofanyika katika viwanja vya gofu vya Sea Cliff Kisiwani Zanzibar jana. Mashindano hayo yalidhaminiwa na NBC ikiwa ni sehemu ya shughuli za kusapoti sekta za michezo na utalii nchini.
Mbunge wa Kenya, Kassim Sawa (kushoto), akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Wateja Rejareja Maalum wa Benki ya NBC, Ashura Waziri baada ya kushiriki mashindano ya kwanza ya gofu mabalozi yaliyodhaminiwa na NBC katika viwanja vya gofu vya Sea Cliff Kisiwani Zanzibar jana ikiwa ni moja ya shughuli za kusapoti sekta za michezo na utalii nchini.

Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Damas Ndumbaro akijiandaa kupiga mpira wakati wa Mashindano ya kwanza ya Golf ya Mabalozi yaliyodhaminiwa na Benki ya NBC ikiwa ni sehemu ya shughuli za kuisapoti sekta ya Michezo na Utalii zinazoendelea kufanyika sehemu mbalimbali nchini. Mashindano hayo yamefanyika katika viwanja vya Sea Cliff kisiwani Zanzibar jana.
Wacheza gofu wakipozi kwa picha pamoja mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushikiano wa Afrika Mashariki pamoja na maofisa wa Benki ya NBC wakati wa mashindano hayo mjini Zanzibar jana.
BENKI ya NBC imedhamini mashindano ya kwanza ya gofu ya mabalozi visiwani Zanzibar huku ikiahidi kuendelea kusapoti sekta ya michezo na utalii visiwani humo kutokana na mchango wake katika maendeleo ya taifa.

Akizungumza wakati wa mashindano hayo katika Viwanja vya Gofu vya Sea Cliff visiwani humo jana, Mkuu wa Kitengo cha Wateja maalumu binafsi wa Benki ya NBC, Ashura Waziri alisema licha ya kuwa michezo husaidia afya kitu ambacho ni muhimu katika uzalishaji mali, lakini pia michezo yenyewe inaweza kuongeza ajira na kuinua uchumi wa wanamichezo na kwa taifa.

“Naihakikishia Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar kwa kupitia Kamisheni ya Utalii kuwa NBC itaendelea kuisaidia kwenye michezo kama tulivyofanya kwa kudhamini gofu ya mabalozi, tunathamini michezo kwa wafanyakazi wetu pia, tunaihakikishia wizara ya michezo pia tutaendelea kusapoti michezo,” akaongeza.

Naye Meneja wa Tawi la NBC mjini Zanzibar, Ramadhani Lesso alisema NBC imekuwa mdau mkubwa wa maendeleo visiewani humo na ndio sababu ya kuitikia wito wa Wizara ya Habari na Utalii kupitia Kamisheni ya Utalii kushiriki katika mashindano hayo kwani wamekuwa wakishirikia kwa muda mrefu aatika kusapoti utalii visiwani humo.

“Kama mnavyofahamu benki yetu ina ATM zisizopungua 7 hapa Zanzibar na zote zinatoa huduma ya Visa ambayo ni maalumu kwa ajili ya wananchi wote lakini zaidi kwa watalii. Kwahiyo utakuta watalii wanafaidika sana wanapotumia mashine zetu za kutolea pesa na mashine nyingine zilizopo mahotelini.

“Watalii ni muhimu sana kwetu ndio maaana tulipopata mualiko huu kutoka kwa Mkurugenzi wa Kamisheni ya Utalii tuliona ni sehemu muhimu sana kwetu kwa ajili ya kuunga mkono serikali kwa upande wa maendeleo na vilevile ikiwa ni sehemu ya michezo kama ilivyo sera ya michezo,” aliongeza.

Pamoja na hayo meneja huyo akatoa wito kwa serikali na wadau wa michezo kuunga mkono juhudi za kusapoti mchezo wa gofu ufundishwe mashuleni na sehemu zote ili watanzania wote waweze kuucheza a kuupenda.

Katika mashindano hayo, ambayo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Mambo na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Damas Ndumbaro, ambaye pia alikuwa mshiriki, Eliah John aliibuka kidedea kwa kushika nafasi ya kwanza huku Issa Mohamed Chaap wote wa visiwani humo kushika nafasi ya pili.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/33gjgim
via
logoblog

Thanks for reading Benki ya NBC yadhamini Gofu ya Mabalozi visiwani Zanzibar

Previous
« Prev Post