Ticker

10/recent/ticker-posts

WAZIRI JAFO AAGIZA KUWAPELEKA WANAFUNZI KATIKA SHULE WATAKAZOZICHAGUA


 WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za mitaa (Tamisemi) Suleiman Jafo akizungumza wakati wa kutoa tunzo  za Elimu kwa wanafunzi, walimu na shule zilizofanya vizuri katika matokeo ya mitihani ya kidato cha sita na darasa la saba 2019.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za mitaa (Tamisemi) Suleiman Jafo amemuagiza Katibu Mkuu Tamisemi, kuwapeleka wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo yao katika shule watakazochagua ili kuwawezesha kutimiza ndoto zao.

Waziri Jafo ameyasema hayo wakati tamasha utoaji tunzo kwa za Elimu kwa wanafunzi, walimu na shule zilizofanya vizuri katika matokeo ya mitihani ya kidato cha sita na darasa la saba 2019 zilizoratibiwa na Global Education Link kwa kushirikiana na Baraza la Mitihani Tanzania.

Amesema, serikali inafanya yote hayo katika kutoa hamasa, kukuza na kuongeza ushindani katika elimu kwani siyo vizuri kukatisha ndoto za vijana hao.

"Yule  kijana Tanzania one nilimsikia anasema anatamani kwenda shule ya sekondari ya Iliboru nitashangaa sana kama hataenda huko, hawa ni vijana special waambieni wachague shule wanazotaka waende kusoma, ..Naomba niwahakikishie, Rais Magufuli anawapenda sana, mtachagua shule zile mnazotaka nyinyi kwenda kusoma, katibu mkuu shughulikiia hilo. Amesema Jafo.

Aidha, amesema kwa, wale wa kidato cha sita kwa kuwa Waziri wa Elimu Profesa Ndalichako yupo basi atalishughulikia hilo.

" Hawa ni vijana special, kwa vile katibu mkuu wa elimu yupo hapa na kuna vijana wa kidato cha sita, msiharibu ndoto za watu. Lazima tujifunze kutafsiri utashi wa watu, nini wanataka hawa vijana.". Amesema.

Aidha, Waziri Jafo amewataka wataalamu wanaotunga miongozo ya elimu kuweka yenye manufaa ambayo itakuwa inaangalia taifa linapoelekea.

"Hizi ni tuzo ya kwanza kutolewa na Serikali kwani vijana na walikumu waliofanya vizuri kwenye mtihani hiyo wanastahili pongezi ili waendelee kufanya vizuri na tunaamini itaongeza ubora zaidi kwa shule zetu kuendelea kufanya vizuri," amesema Jafo.

Jafo amesema baada ya kupata wazo la utoaji wa tuzo hiyo kazi ya kuratibu walipewa Global Education Link kwa kushirikiana na Baraza la Mitihani Tanzania.

Amesema, tuzo hizo mpya ni za historia ndani ya nchi . Kwani Serikali ya Awamu ya Tano kwa upana wake imeamua kufanya kitu cha pekee kwa kuwatambua walimu na wanafunzi waliofanya vizuri kwa kiwango kikubwa.

Amesema, Serikali ilikuwa ikitoa zawadi mbali mbali huko nyuma lakini utaratibu huu mpya wa tuzo ambao ndio mara ya kwanza unafanyika, utaongeza chachu ya elimu na kuiwezesha nchi kufikia katika uchumi wa viwanda. 

"Mafanikio makubwa ya kuwekeza kwenye elimu yanaonekana hasa katika ufaulu kwa ngazi zote kuanzia darasa la saba hadi kidato cha sita, mfano mwaka jana, katika shule bora 100, shule 64 zilikuwa za umma na shule 52 zilikuwa za kata, hii ilikuwa ni mara ya kwanza ndipo nikaamua kutambua shule bora. Amesema Jaffo

Aidha amesema, mwakani licha ya kuthamini waliofanya vizuri, pia mwakani vijana watakaofanya vizuri katika fani ya michezo,  wataingizwa katika tuzo hizo ambapo watabainisha mchezaji na msanii wa mwaka ili kutambua kazi kubwa wanayoifanya kwani elimu ni pamoja na michezo

Katika tuzo hizo zilizojumuisha, walimu wakuu, walimu wa masomo, shule, wilaya na mikoa iliyoongoza kwa ufaulu huo pia wasimamizi wa mitihani kutoka mikoa mbali mbali nao wamejumuishwa.

Kwa upande wake, mratibu mkuu wa tuzo hizo, Mkurugenzi wa Global Education Link Abdalmalik Mollel amesema ili walimu na wanafunzi wafanye vizuri darasani wanahitaji motisha.

" Watoto wengi nimeongea nao hawana matamanio makubwa ya mamilioni, wanataja tu aina za shule wanazozitaka, waende,  pia wale wa vyuo vikuu wanasema teyari wamepata nafasi vyuoni ila wanaomba bodi ya mikopo isiwasahau kuwapa mikopo na mimi kama mratibu ninasema wanastahili. Walimu nao hawako nyuma wanahitaji wakiwa wamefanya vizuri serikali isimame na kusema tunakutambua hongera., amesema Mollel.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania Charles Msonde amesema utoaji wa tuzo hizo utaongeza kiwango cha ufaulu.

"Ushindani wa tuzo hizi ni heshima kwa Baraza la Mitihani," amesema.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2JvAXSX
via

Post a Comment

0 Comments