SEMINA KWA WANAHABARI KUHUSU KAMPENI SHIRIKISHI YA SURUA RUBELLA SINGIDA

  Masama Blog      

 Mratibu wa Afya ya Uzazi na Mtoto Mkoa wa Singida, Christoweru Barnabas, akitoa mada katika semina ya waandishi wa habari kuhusu kampeni shirikishi ya Surua  Rubella.
 Waandishi wakiwa kwenye semina hiyo 
 Kaimu Mganga Mkuu Mkoa wa Singida, Ernest Mugetta akizungumza kwenye semina hiyo.
 Mratibu wa Afya ya Uzazi na Mtoto Mkoa wa Singida, Christoweru Barnabas, akisisitiza jambo kwenye semina hiyo. Kulia nMratibu wa Chanjo Mkoa wa Singida, Jadili Mhanginonya.
 Mratibu wa Magonjwa yanayozuilika na Chanjo kutoka Wizara ya Afya,  Honest Nyaki akizungumza.
 Majadiliano yakifanyika.
Picha ya pamoja

Na Dotto Mwaibale, Singida

MKOA wa Singida umelenga kutoa chanjo ya Surua- Rubella kwa watoto 225,586 na polio watoto 119,198 na kuhakikisha wanafikisha asilimia 100 ya kutoa chanjo hizo.

Hayo yalisemwa jana na Mratibu wa Chanjo Mkoa wa Singida, Jadili Mhanginonya wakati akizungumza na waandishi wa habari katika semina kuhusu kampeni shirikishi ya Surua-Rubella 2019.

"Tunataka mkoa wetu wa Singida tufikie asilimia 100 ya chanjo hiyo kwani tumejipanga vizuri kwa kazi hiyo" alisema Mhanginonya.

Alisema chanjo ya kitaifa ya mwaka 2014 kwa mkoa huo ilikuwa ni asilimia 98 ambapo waliwafikia watoto 615,000 na walikuwa kuanzia umri wa miezi 9-15 

Alisema maandalizi yote ya kampeni hiyo ya siku tano itakayoanza kesho nchi nzima kwa mkoa wa Singida yamekamilika kwa kupeleka vifaa maeneo yote yaliyotengwa na timu ya watendaji ipo tayari kwa kazi hiyo.

Alisema kwa mkoa huo wanatarajia kuzindua kampeni hiyo Halmashauri ya Wilaya ya Itigi na itazinduliwa na Mkuu wa Mkoa Dkt.Rehema Nchimbi viwanja vya Square Polisi.

Mratibu wa Afya ya Uzazi na Mtoto Mkoa wa Singida, Christoweru Barnabas alisema waandishi wa habari wanawajibu wa kuhabarisha jamii kuhusu madhara ya ugonjwa wa Surua na Rubella.

"Ninyi wanahabari ndio tegemeo kubwa katika kampeni hii mnatakiwa kuhabarisha umma kuhusu uwepo wa chanjo ya kukinga ugonjwa wa kupooza (polio) na umri sahihi wa kupata chanjo ya Surua, Rubella na Polio" Barnabas.

Barnabas alitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi wote mkoani Singida kujitokeza kwa wingi kupeleka watoto wao kupata chanjo hiyo.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2MOyzrd
via
logoblog

Thanks for reading SEMINA KWA WANAHABARI KUHUSU KAMPENI SHIRIKISHI YA SURUA RUBELLA SINGIDA

Previous
« Prev Post