DOWNLOAD APP YETU HAPA

OSHA YAPONGEZWA KWA KUONDOA URASIMU

  Masama Blog      
Mkuu wa Wilaya ya Longido, Mhe. Frank Mwaisumbe amewapongeza Wakala wa Afya na Usalama Mahala Pa Kazi (OSHA)  kwa kubadili mfumo wa utendeji kazi wake na kuondoa urasimu wa utendaji kazi, kwani urasimu hupelekea shughuli nyingi kukwama kupelekea wawekezaji wengi kukimbia nchini kutokana na vikwazo. 

Mwaisumbe aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo, amesema hayo jiji Arusha wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Wakaguzi wa Usalama na Afya kutoka OSHA na WCF, amesema juhudi za kupunguza tozo kumeisaidia OSHA kuweza kuwafikia Wawekezaji wengi zaidi na hivyo suala la Usalama na Afya Mahali Pa kazi kuanza kutekelezwa na kuzingatiwa  na Waajiri wengi hapa nchi.

“Nimefarajika kusikia kwamba, mmeendelea kuboresha huduma zenu, hilo ni jambo jema. Waajiri wengi nchini hawatapendi kuona urasimu, wengi wao wawekezaji wakiona kuna urasimu huondoka na kutafuta sehemu zingine ili waweze kuwekeza” amesema Mhe. Mwaisumbe .

Mhe. Mwaisumbe amesema juhudi hizi ambazo zimefanywa na OSHA zimekuja kipindi kizuri hasa kipindi hiki nchi inapotekeleza miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo Miradi ya Umeme, Ujenzi wa Barabara, Madaraja, ambapo watu wengi huajiri.

Naye Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda amesema mafunzo hayo yameandaliwa kwa lengo la kuwaongezea uwezo watumishi wa Umma kwa lengo la kutoa huduma bora katika maeneo yao ya kazi. Amesema Wakala unaendelea kuboresha huduma zake, hivyo mafunzo hayo yataongeza ufanisi kwa wakaguzi wawapo kazini.

Khadija amesema yakuwa wakati nchi inaendelea kupiga hatua mbalimbali za kiuchumi na mabadiliko mbalimbali ya Kiteknolojia duniani, mafunzo kama haya yatakuwa muafaka, yataenda sambasamba na kuwafunza wakaguzi mbinu mpya za kukabiliana na mabadiliko hayo pamoja na changamoto.

“Wenzetu hawa huko kwao masuala ya usalama na Afya yanazingatiwa na yanapewa kipaumbele, sasa ujuzi ambao wakaguzi wataupata kutoka kwa wataalamu hawa yatasaidida kuboresha utendaji kazi wetu, na mbinu mpya za kuweza kufanikisha zoezi zima la kufanya kaguzi za usalama na Afya,” amesema Bi Mwenda.

Naye, Mjumbe wa Shirika la Workplace Health without Borders (WHWB), Aristides Medard kutoka Tanzania ambao ni Waratibu wa Mafunzo hayo kwa kushirikiana na OSHA kwa upande wa Tanzania amesema lengo kubwa la taasisi hiyo ni kuhakikisha linatoa mafunzo  yanayolenga kuondoa changamoto mbalimbali za usalama na Afya Mahali pa kazi duniani ambazo hujitokeza.

Mafunzo haya ya wiki moja yameandaliwa na OSHA kwa lengo la kuwajengea uwezo wa wakaguzi wa OSHA pamoja na WCF, namna bora ya kufanya kaguzi, na yanaendeshwa na wakufunzi kutoka CANADA,MAREKANI na UBELGIJI kutoka shirika la kimataifa la Workplace health without Border (WHWB).
 Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda akizungumza na Wakaguzi wa Usalama na Afya kutoka OSHA na WCF wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Wakaguzi hao jijini Arusha.
Mkuu wa Wilaya ya Longido, Mhe. Frank Mwaisumbe akizungumza na Wakaguzi kutoka OSHA wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa Wakaguzi hao ambapo amewapongeza Wakala wa Afya na Usalama Mahala Pa Kazi (OSHA).
 Baadhi ya Wakaguzi wa OSHA wakiwa kwenye ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo jijini Arusha.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2Bb8a1t
via
logoblog

Thanks for reading OSHA YAPONGEZWA KWA KUONDOA URASIMU

Previous
« Prev Post