DOWNLOAD APP YETU HAPA

MKANDARASI AAGIZWA KUMALIZA UJENZI WA MADARASA YA GHOROFA NDANI YA MUDA ULIOPANGWA

  Masama Blog      
Na Jusline Marco -Arusha

Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi Bw.Joseph Masawe amemuagiza mkandarasi aliyepewa kazi ya ujenzi wa madarasa 4 ya Ghorofa kwenye Shule ya Sekondari Sombetini kuhakikisha ujenzi huo unakamilika mapema ndani ya muda wa nyongeza aliopewa kwani ameonekana akichelewesha ujenzi kinyume na mkataba unavyoelekeza.

Masawe ametoa agizo hilo wakati alipokuwa kwenye ziara iliyoongozwa na kamati ya Siasa ya Halmashauri kuu wilaya ya Arusha ya ukaguzi wa miradi ambayo imetekelezwa na ilani ya chama hicho kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 leo Tarehe 1 Octoba 2019 Mkoani Arusha.

Akizungumzia miradi jiuo Masawe amesema kuwa ziara hiyo ni ya kawaida na ina lengo la kuhakikisha yale ambayo yaliahidiwa chini ya ilani ya Chama cha mapinduzi kupitia Rais Dkt. John Pombe Magufuli yanatekelezwa kwa wakati.

Aidha miradi 10 iliweza kutembelewa ni pamoja na mradi wa Tenki la maji ESAMI, Ujenzi wa jengo la wodi ya wazazi hospitali ya wilaya, Matundu ya vyoo 20 shule ya msingi Murriet Darajani, Matundu ya vyoo 10 shule ya msingi sokoni I, Ujenzi wa Daraja la Shaulalu kata ya Sokon 1.

Miradi mingine ni ujenzi wa madarasa 4 ya ghorofa shule ya Sekondari Sombetini,ujenzi wa uzio katika kituo cha afya daraja II,ujenzi wa barabara ya Masjid Quba na barabara ya Sanawari pamoja na Vikundi vya wanawake, vijana na wenye ulemavu vilivyopewa mikopo kata ya Ngarenaro.

Pamoja na hayo amesema chama cha mapinduzi kiko makini katika kuhakikisha changamoto zote zinatatuliwa pamoja na yale waliyoahidi kupitia serikali ya awamu ya tano yanatekelezwa ikiwemo suala la Elimu, Afya, Miundombinu ya barabara pamoja na maji.

Hata hivyo Kamati hiyo imeridhishwa na ujenzi wa matundu 30 ya vyoo katika shule mbili za msingi Murriet na Sokon 1 ambayo yako katika hatua za umaliziwaji.

Pia kamati hiyo ya utekelezaji wa chama cha Mapinduzi kimewapongeza watendaji wa serikali ambao wamekuwa makini kusimamia miradi ya maendeleo hasa katika kuelekea kwenye kipindi hiki cha uchaguzi wa serikali za mitaa ambapo amesisitiza ushirikiano baina ya watumishi na wakandarasi ili kupelekea miradi kutekelezwe kwa wakati na kuepusha vikwazo pindi inapoanza.
Kamati ya Siasa ya halmashauri kuu wilaya ya Arusha ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi Bwana Joseph Masawe wakitembelea baadhi ya miradi ambayo imetekelezwa na ilani ya chama hicho.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2pr7sdR
via
logoblog

Thanks for reading MKANDARASI AAGIZWA KUMALIZA UJENZI WA MADARASA YA GHOROFA NDANI YA MUDA ULIOPANGWA

Previous
« Prev Post