DOWNLOAD APP YETU HAPA

Mgogoro wa mudamrefu wa kugombea mali katika familia ya marehemu bilionea erasto Msuya wachukuwa sura mpya

  Masama Blog      
Na Woinde shizza Michuzi Tv , Arusha 

Mgogoro wa Muda mrefu uliokuwa ukifukuta baina ya familia za Marehemu bilionea Erasto Msuya wa kugombea Mali umechukua sura mpya mara baada ya serikali ya Mkoa kuingilia kati kwa lengo la kupata suluhu ya kudumu nje ya Mahakama.

Mgogoro huo ambao umedumu kwa takribani miaka 7 tangia kifo cha Marehemu mwaka 2013, upande wa wazazi wa marehemu Erasto msuya na upande wa Mke wa marehemu  Erasto aitwaye Miriam  Erasto ambaye kwa sasa yupo mahabusu Gerezani kwa tuhuma ya mauaji ya WiFi yake,wameshindwa kuelewana juu ya rasilimali zilizoachwa na marehemu.

Akiongea na familia hizo katika nyumba aliyokuwa akiishi Marehemu Erasto iliyopo Kwa Iddy wilayani Arumeru,Mkuu wa wilaya hiyo Jerry Muro amewataka watoto wa marehemu  waliokuwa wameikimbia nyumba ya marehemu baba yao wakihofia kuuawa kurejea katika nyumba hiyo kuanzia Leo wakati wakiendelea na utatuzi wa mtafaruku uliopo.

Aidha Muro amezitaka pande hizo mbili kufika ofisini kwake siku ya jumatatu SAA 4 asubuhi wakiwa wameambatana na vielelezo mbalimbali ili kufikia mwafaka wa mgogoro huo nje ya Mahakama.

"Si nia ya serikali kuingilia jambo lililopo mahakamani ila kama serikali tunamamlaka ya kusuluhisha jambo iwapo pande zote zipi tayari kuketi kwani suala la kutafuta msindi mahakamani si suluhu ya kuleta amani" Amesema Muro

Akiongea mgogoro huo mtoto mkubwa wa marehemu , aitwaye Kervin Erasto  alimweleza mkuu huyo wa Wilaya kuwa wazazi wa marehemu baba yake( bibi) aitwaye Ndeshu Msuya na babu yake aitwaye Elisaria Elia Msuya pamoja na shangazi zake wanataka kumpokonya Mali za Marehemu baba yake .

Akijibu tuhuma hizo,Mama wa marehemu Erasto,Ndeshu Msuya amesema kuwa wao kama wazazi wa marehemu Erasto hawana nia ya kutaka urithi wa mali yoyote ya marehemu  mtoto wao ila wanasikia uchungu kuona Mke wa Erasto akiuza Mali ovyo za Marehemu mtoto wao ili kumaliza suala la kesi ya mauaji inayomhusu wakati ugawanyo wa Mali bado haujafikiwa.

Mama huyo amedai kuhofika watoto wa marehemu kupoteza rasilimali hizo kutokana na Mali hizo ndugu wa Mke  kujimilikisha ambao wamejipa kipaumbele kusimamia jambo ambalo linawapa mashaka kwamba huenda watoto hao wakadhulumiwa.

Naye baba wa marehemu aitwaye Elisaria Msuya amesema  madai yanayotolewa kuwa amejimilikisha mgodi wa marehemu Erasto hayana msingi wowote kwani wakati anamzaa Erasto alikuwa anamiliki migodi huko Mererani na ubilionea wa Msuya umetokana na yeye kumpa mgodi wa kuchimba madini ya Tanzanite.

Marehemu Erasto alifariki agosti,7mwaka  2013 kwa kupigwa risasi zaidi ya 20 eneo la Mijohoroni,wilaya ya Hai ,mkoani Kilimanjaro na watu ambao baadae walikamatwa na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela Mara baada ya Mahakama kuwatia hatiani.
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro (pili kushoto) akiwa na familia ya marehemu bilionea Erasto Msuya


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/33Ary4a
via
logoblog

Thanks for reading Mgogoro wa mudamrefu wa kugombea mali katika familia ya marehemu bilionea erasto Msuya wachukuwa sura mpya

Previous
« Prev Post