Ticker

10/recent/ticker-posts

TANESCO wawaomba radhi wateja wake wa Dar es Salaam


Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawaomba radhi Wateja wake wa Mkoa wa Dar es salaam kwa kukosa huduma ya umeme kwa siku za hivi karibuni kutokana na maboresho makubwa yanayohusisha matengenezo kinga ya mashine 3 za Kituo cha Ubungo II, pamoja na uwekaji wa transfoma kubwa la MVA 300 kwenye Kituo cha kupoza umeme cha Ubungo ili kukiongezea uwezo na kwenda sambamba na ukuaji wa mahitaji ya jiji la Dar es Salaam.

Kabla ya matengenezo kuanza mnamo Januari 2019 Kituo hiki cha kupoza umeme cha Ubungo kimekuwa kinapokea umeme kutoka katika vituo vya Uzalishaji umeme vilivyopo upande wa msongo wa kilovolti 220 kupitia transfoma mbili zenye uwezo wa MVA 150 kila moja, zenye kupokea umeme wa msongo wa Kilovolti 220 na kuushusha hadi kuwa msongo wa Kilovolti 132 katika transforma namba sita na namba saba za kituo cha Ubungo na vituo vya uzalishaji umeme vilivyoungwa kwenye msongo wa kilovolti 132 ambavyo vimeungwa moja kwa moja kwenye mfumo mkuu wa usambazaji umeme kwa Dar es Salaam na Zanzibar.

Kutokana na matengenezo yanayoendelea vituo vya uzalishaji umeme vilivyoungwa kwenye msongo wa kilovoti 132 na 33 vimekuwa nguzo kubwa ya upatikanaji wa umeme. Vituo hivyo ni Ubungo II na Tegeta.

Shirika kupitia wataalamu wake tayari limefanya jitihada kubwa za kupunguza athari za upungufu wa upatikanaji wa umeme kwa wakaazi wa Dar es salaam na Zanzibar kwa kufanya yafuatayo:
Mosi, Kufungua laini ya msongo wa kilovoti 132 kati ya Kilimanjaro na Hale: Hili hufanyika ili kutoruhusu umeme wa kutoka Dar es Salaam na Morogoro kwenda Kilimanjaro hivyo Mkoa huu kuchukulia kwenye upande wa msongo wa kilovolti 220 kutoka Arusha.

Pili, Kuwezesha upatikanaji wa umeme katika baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Dar es salaam, kwa kuunga baadhi ya njia za Usafirishaji umeme kutoka Kituo cha Kinyerezi, Gongolamboto hadi Mbagala ili kuwezesha maeneo hayo kupata umeme bila kupitia kituo cha Ubungo ambacho kipo katika matengenezo.

from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/2SWABeW
via

Post a Comment

0 Comments