Ticker

10/recent/ticker-posts

Fiesta Kukiwasha Leo Viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar

WAPENZI wa burudani leo Jumamosi watakuwa na shangwe pale Viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar wakati Tamashala Fiesta litakapokuwa l i k i r i n dima huku mastaa kibao wakitarajiwa kutoa burudani.

 

Awali tamasha hili lilitarajiwa kufanyika Novemba 24, mwaka huu kwenye Viwanja vya Leaders, Dar lakini lilisitishwa kutokana na sababu mbalimbali.

Akizungumza na Championi Jumamosi, mmoja wa waratibu wakuu wa tamasha hilo, Hamisi Mandi ‘B12’, alisema kuwa leo Jumamosi kutakuwa na sehemu moja tu ya kwenda hususan

kwa wale wapenzi wa burudani nayo ni kwnye Tamasha la Fiesta kwani wasanii wote wakubwa watapanda jukwaani kupafomu.

“Tumeamua kuipa heshima Fiesta baada ya kuahirisha ya kwanza katika Viwanja vya Leaders Club pale Kinondoni na heshima hii itajidhihirisha kesho (leo) kufuatia makamuzi ya nguvu yatakayoshushwa na wasanii wa hapa nchini.

“Kuna mastaa kibao watapanda jukwaani kama AliKiba ambaye ndiye atakayeongoza jahazi pia Kundi la Nako 2 Nako linaloongozwa na Joh Makini na wenzake, wakongwe kama Juma Nature, Fid Q, Chege, Mr Blue, TID, Soggy Doggy na wengine watapanda kuwapa burudani mashabiki zao.

 

“Hatujamaliza, pia kuna akina Jux, Vanessa Mdee, Rich Mavoko, Msami, Maua Sama, The Mafi k, Christian Bella, Rosa Ree na wengine wengi watapanda kwenye jukwaa la Fiesta kukamilisha burudani.

 

“Maandalizi ya shoo hiyo yamekamilika kwa asilimia 100 na kinachosubiriwa ni muda wa kuanza kudondosha burudani tu ili watu waweze kuburudisha nafsi zao baada ya ile ya kwanza kushindwa kufanyika,” alisema B12.

The post Fiesta Kukiwasha Leo Viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar appeared first on Global Publishers.



from Global Publishers http://bit.ly/2LuuFmz
via

Post a Comment

0 Comments