Ticker

10/recent/ticker-posts

Aliyekuwa Makamu wa rais wa kampuni ya Acacia na Wenzake Waendelea Kusota Rumande

Aliyekuwa makamu wa rais wa kampuni ya Acacia, Deo Mwanyika na wenzake watakula Sikukuu ya Krisimasi na Mwaka Mpya gerezani baada ya upande wa mashtaka kuieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa upelelezi wa kesi yao bado haujakamilika.

Wakili wa Serikali, Simon Wankyo amedai hayo leo Ijumaa Desemba 21, 2018 kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.

Hakimu Mkazi Mfawidhi, Kelvin Mhina ameahirisha kesi hiyo  hadi Januari 4, 2019.

Mbali na Mwanyika, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni meneja uhusiano wa mgodi wa Bulyanhulu,  Alex Lugendo; mkurugenzi mtendaji wa Pongea, North Mara na Bulyanhuku Assa Mwaipopo; kampuni ya mgodi ya Pangea, North Mara, Exploration na Bulyanhulu.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 39, yakiwemo ya utakatishaji na kukwepa kodi zaidi ya Dola 112 milioni za Marekani.

Washtakiwa hao pia wanakabiliwa na mashtaka matatu ya kula njama, saba ya kughushi, 17 ya utakatishaji wa fedha, kuwasilisha nyaraka za uongo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), shtaka moja la  kuongoza uhalifu wa kupangwa, mashtaka manane ya kukwepa kodi na moja la kutoa rushwa.


from MPEKUZI http://bit.ly/2EBEFsE

Post a Comment

0 Comments