Ticker

10/recent/ticker-posts

Majengo Yaliyojengwa Kwenye Hifadhi ya Barabara Masaki Kubomolewa

Miongoni mwa maeneo maarufu yatakayobomolewa kwa kutekeleza agizo la Wakala wa barabara za mijini na vijijini(TARURA) ni Elements, Eaters Point, Didis, Buckets, Jackies, Shangrilla na Mishkaki

Meneja TARURA Wilaya ya Kinondoni, Leopold Runji amesema kama hawataondoa wenyewe kama walivyokubaliana wataondolewa kwa nguvu

Amesema "Tulikubaliana tangu Juni, 2018 lakini wamedharau kuondoka au kubomoa wao wenyewe, juzi tumeweka ‘X’ kuwakumbusha hatuna muda wa kuwapa waondoe sasa"

Kuhusu wanaodai wamepewa vibali na Manispaa Vya kuendelea kufanya shughuli zao amesema, “Kikao walikaa na TARURA, siyo manispaa na TARURA ndiyo inayoshughulika na barabara."