Ticker

10/recent/ticker-posts

Utafiti: Je Unajua Jeraha la Mchana Hupona Haraka Kuliko Lile la Usiku


Utafiti: Je Unajua Jeraha la Mchana Hupona Haraka Kuliko Lile la UsikuWanasayansi nchini Uingereza wamegundua kwamba majeraha ya kukatwa na kuchomeka hupona haraka yanapopatikana mchana ikilinganishwa usiku.
Wanasema kwamba ni kutokana na mwili unavyohisi kulingana na muda.
Utafiti huo unasema kuwa seli za ngozi ya mwanadamu hubadilisha tabia yake kulingana na muda huku protini zinazohitajika kurekebisha majeraha hayo zikifanya kazi vizuri wakati wa mchana.
Jeraha la kuchomeka nyakati za usiku lilichukua siku 28 kupona ikilinganishwa na siku 17 za jereha la wakati wa mchana.
Watafiti walitaja tofauti hiyo kuwa kubwa huku wakiongezea kwamba wanaweza kuharakisha watu kupona kwa kutumia dawa za steroids ambazo hubadilisha muda wa mwili.

Utafiti uliochapishwa katika jarida la Sayansi uliwahoji wagonjwa 118 katika kitengo cha wagonjwa waliochomeka nchini Uingereza.
Ulionyesha muda wa kupona wa 11 kati ya watu nyakati za mchgana na usiku.
Matokeo ya mahabara yalionyesha kuwa seli za ngozi kwa jina Fibroblast zilikuwa zikibadili uwezo wake katika kipindi cha saa 24

Seli hizo ndizo za kwanza zinazokimbia katika jeraha hilo ili kufunga kidonda.
Nyakati za mchana huwa zinafanya kazi sana na hupoteza nguvu hiyo nyakati za usiku.
Daktari O'neil mmoja ya watafiti aliambia BBC ''ni kama kukimbia mita 100''. Mkimbiaji hujiandaa kutoka , kawaida atamshinda yule aliyesimama akijiandaa kukimbia''.