Ticker

10/recent/ticker-posts

PICHA: Mamia wafunga barabara Kilimanjaro Ili wamsalimie Rais Magufuli..Shududia hapa

Rais John Pombe Magufuli Aprili 29, 2017 aliwasili Moshi mkoani Kilimanjaro ambapo atafanya ziara ya kikazi kwa muda wa siku tatu.Alipofika Eneo la Bomang'ombe wilayani Hai,Wananchi walifunga Barabara Wakitaka Awasalimie ambapo wananchi walibeba majani aina ya Masale na kisha alisimama na Kuwaambia ''Ninajua maana ya haya Majani(Masale)..Na mimi nimewasamehe,najua nanyi mmenisamehe..Pia baada ya Mwendo Mdogo wananchi wa Eneo la Kwasadala walizuia msafara wa Rais Magufuli ambapo napo alisimama na kuwasalimia amabapo alitoa agizo la kufuta kodi zote za mazauzo ya ndizi au biashara ndogo ndogo na kusema kuanzia sasa wanaotakiwa kulipa ushuru ni wafanyabiashara wakubwa tu katika Masoko mkoani Humo.

Sambamba na ziara hiyo, Rais Magufuli kwa Mara ya Kwanza Aliambatana na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa,Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan,Mawaziri na Watendaji wakuu wa Serikali ikiwa wanatarajiwa kuhudhuria sherehe za Sikukuu ya Wafanyakazi (Mei Mosi) ambapo Rais Magufuli atakuwa mgeni rasmi leo .