Ticker

10/recent/ticker-posts

JACK Wolper: Sijawahi kuachwa Kwenye Maisha Yangu

Msanii wa filamu Jacqueline Wolper amefunguka kuizungumzia ishu ya kuachana na aliyekuwa mpenzi wake, Harmonize.
Muigizaji huyo amedai hana msongo wa mawazo kutokana na tukio hilo huku akidai hajaachwa kama baadhi ya watu kwenye mitandao wanavyodai.
Jackline-Wolper
“Kuachwa ndio nini? kweli ulilolijua ni kama usiku wa giza,” Wolper alikiambia kipindi cha U Heard cha Clouds FM. “Kwenye maisha yangu sijawahi kuachwa, sina kabisa record hiyo sema sitakagi kufanywa mjinga. Yeye kama amezungumza ishu ya kuachana na mimi, mimi sitaki kulizungumzia kwa sababu na mambo yangu mengi ya umuhimu nafanya,”
Harmonize hivi karibuni alifunguka na kuweka wazi kwamba hayupo tena kwenye mahusiano ya mrembo huyo kutoka tasnia ya filamu huku akishindwa kueleza sababu.