Ticker

10/recent/ticker-posts

Jinsi ya kupata kitu unachokitaka na kwa wakati muafaka

Jinsi ya kupata kitu unachokitaka kwa wakati muafaka

Wengi wetu huwa tuna fikra na imani potofu zinazokwamisha mafanikio ya malengo yetu binafsi. Huwa kama vizuizi vya njia ya mafanikio kati yetu na maisha tunayoyataka. Nina imani kila mmoja wetu ana hulka ya kumiliki kitu au vitu anavyovitaka. Ni rahisi sana kutafakari na kutamani vitu unavyovitaka kuliko kuvifanikisha.

Kama ingekuwa rahisi kupata vitu unavyovitaka, nadhani kusingalikuwa na haja ya kuhitaji chochote – Si Ndio? Ukweli ni kwamba hakuna njia iliyonyooka ya kuvipata unavyovitaka bali leo nitakushirikisha baadhi ya mbinu muhimu zitakazokusaidia kurahisiha ufanikishaji wa kupata kitu au vitu unavyovitaka katika namna moja au nyingine.
Hii inaweza kuonekana kama jambo la kawaida sana, lakini mengi wetu wana tatizo la kushindwa kuomba kitu wanachokitaka. Je, unataka kulipa kuongezewa malipo? Je, unataka kujua kama mpenzi uliyempata anakupenda kwa dhati? Jiamini, nenda kwa muhusika, na kisha umuulize. Hii inaweza kuwa njia rahisi kabisi ya kupata unachokitaka.
Watu wengi huchelewa kupata vitu wanavyovitaka kwasababu ya kupoteza muda mwingi katika kusubiria “wakati muafaka.” Naam, kama utakuwa mtu wa kusubiri wakati muafaka, kuna wakati mwingine utalazimika kupoteza muda mwingi katika subira yako. Wakati mwingine unapaswa kukifuata tu kitu na kukipata. Isipokuwa kama una sababu nzuri na ya kweli ya kusubiri.
Moja ya njia mahususi ya kufanikisha kupata kitu unachokitaka ni kufanya mpango madhubuti tena kwa kuuandika katika kitabu chako cha kumbukumbu. Orodhesha malengo yako kisha uyaandike chini. Kuandika lengo lako katika karatasi ndio dhamira kuu hapa. Na kwa kila lengo ulilonalo, jiwekee mpango wa utekelezaji wenye utaratibu unaoeleweka wa kutekeleza malengo yako, pia hakikisha unalifanyia kazi lengo lako kila inapoitwa leo.
Zingatia kupata unachokitaka. Epuka vikwazo visivyo vya lazima, zingatia muda na pia zielekezee nguvu zako katika utekelezaji wa kupata unachokitaka. Na usijilinganishe na watu wengine – Hiyo ni sawa na kujifungulia akaunti ya matatizo.Weka mkazo juu yako mwenyewe na juu ya kile unachoweza kukifanya kutekeleza malengo yako.
Jua unachokitaka, kwa marefu na mapana. Jenga picha akilini mwako kuwa umekipata unachokitaka na kisha jiaminishe kuhusu jambo hilo. Ishi ukiwa na fikra chanya kuwa utapata unachokitafuta. Bila shaka, huwezi kuishia kuamini tu bali utatakiwa ufanye kazi kwa bidii, maarifa na uaminifu mkubwa ili ufanikishe malengo yako.
Tenga muda fulani kila siku kujenga taswira ya maisha baada ya mafanikio ya kile unachokitafuta. Jenga akilini mwako kuwa umekipata kile ulichokuwa unakitafuta. Kwa kufikiria na kukumbuka mafanikio ya lengo lako inakupa urahisi wa wewe kulifikia lengo lako. Vilevile kwa kujijengea taswira ya mafanikio akilini mwako, inakufanya ujiamini na kuamini kuwa unaweza kuyafikia malengo yako.
Jenga uhusiano na watu madhubuti. Jumuika na watu ambao tayari wapo kwenye nafasi unayoitaka, au wamepata mafanikio ya kitu unachokitaka, watakuwa msaada wa pekee sana kwako. Ni jambo jema daima kuwa na uhusiano na urafiki chanya  hasa linapokuja suala la kufikia malengo yako – hasa katika kazi yako.
Ndiyo, mambo yajayo – daima huwa yanatia hofu. Vipi kama usipofanikiwa kupata kitu unachokitaka? Vipi kama ukishindwa? Na maswali mengine mengi kama hayo. Cha msingi ni kutoruhusu hofu yoyote ikuzuie kutekeleza mipango yako. Lakini, vipi kama ukifanikiwa kupata kile unachotaka? Vipi kama ukikipata? Ukweli ni kwamba mis siyajui mawazo yako juu yamafanikio yako mwenyewe, lakini kwa upande wangu mimi nachagua kuishi na maswali ya Vipi kama nikifanikiwa?
Wakati mwingine unatakiwa ukubaliane na matokeo ya kile unachokipata.  Huwezi kuwa unapata kila kitu katika hali unayoitaka daima. Kama umefanya kazi kwa bidii, maarifa na uaminifu wako, na bado ukajikuta haujafanikisha lengo lako, Usikate tamaa! Kubaliana na hali halisi kisha songa mbele kwa kuweka lengo jipya na kufuata mpango wa utekelezaji.
$ Omba
$ Achana na tabia ya kusubiri “wakati muafaka”
$ Fanya mpango
$ Zingatia
$ Amini –
$ – na Uvutie taswira
$ Jumuika na ujenge uhusiano
$ Chukua hatua sasa
$ Kubaliana na matokeo kisha songa mbele