Ticker

10/recent/ticker-posts

ZIARA YA RAIS KIKWETE YAZAA MATUNDA NCHINI KENYA..ANGALIA HAPA TULICHOPATA

Nchi ya Kenya itakuwa mteja mkubwa wa gesi ya Tanzania pindi itakapoanza kuuzwa nje ya nchi, hii ni kwa mujibu wa rais Uhuru Kenyatta ambaye aliyasema hayo juzi mjini Nairobi wakati wa ziara ya siku tatu ya Rais Kikwete, ambaye alikuwa kwenye ziara ya kiserikali nchini humo.
“ Tumekuwa marafiki wa muda mrefu, leo tunajisikia furaha kubwa kuagana na rafiki wa muda mrefu na mtu muhimu kwa Kenya.Tunajivunia kuwa naye na tuna deni kutokana na uhusiano wetu mkubwa,” Uhuru alisema
Alimwagia sifa Rais kikwete kwa kuimarisha jumuiya ya Afrika Mashariki na biashara kati ya Tanzania ya Kenya ambayo imefikia nusu kwa nusu. 
“katika utawala wako pia umesimamia sana masuala ya miundombinu ya kuunganisha nchi zetu. Barabara ya Arusha- Athi uliyoizindua na rais mstaafu Mwai Kibaki na ile ya juzi ya Voi-Arusha ambayo itaunganisha na bandari ya Mombasa ni ushahidi tosha wa jinsi ya kuimarisha biashara kati ya nchi zetu," aliongeza.
Rais Kenyatta alisema upatikanaji wa gesi nchini Tanzania utasaidia kukuza uchumi wa nchi yake kwa kupata nishati ya umeme kwa bei nafuu.
"Maendeleo mapya katika mradi wa gesi ni eneo jingine ambalo Kenya itafaidika nalo, kwani tutanunua kwa bei rahisi na tutakuwa na nishati inayoaminika na hivyo kusaidia nchi yetu kiuchumi na kijamii.asante sana kwa kazi nzuri”.