Ticker

10/recent/ticker-posts

BONNAH KALUA....KUMBE HUYU NDIYE ALIYEMGARAGAZA WAZIRI MAKONGORO MAHANGA HUKO SEGEREA KURA ZA MAONI

Anaitwa Bonnah Kaluwa,ambaye ni Diwani wa Kata ya Kipawa..ni dada mwenye bidii kwa kila anachokifanya,asiyekata tamaa..alistahili kushinda kwani uwezo anao,nguvu anazo na anweza kutekeleza jukumu lolote kwa wakati...Kitaaluma ni mhitimu wa kozi ya Utawala na mahusiano ya kimataifa toka chuo cha kimataifa cha diplomasia,yaani ana cheti kinachotambulika kama Postigraduate in Management of Foreign Relations(PGD-MFR)...ambapo akiwa katika chuo hicho cha kimataifa aliweza kuchaguliwa kuwa katibu wa CCM uchumi na Fedha wa tawi la chuo hicho pia aliweza kupewa nishani ya uongozi bora..
Diwani wa kata ya kipawa jijini Dar es Salaam Mhe.Bonnah Kaluwa kipindi anasoma Chuo cha Kimataifa cha Diplomasia akiwa na Kennedy  Ndosi (Kiongozi Bora)
ambapo naye alishinda tuzo ya mwanafunzi aliyetoa mchango mkubwa kwa wanafunzi wenzake katika chuo cha Diplomasia ambapo alimaliza kozi ya Post graduate in management of Foreign Relations mwaka 2013/2014.

Masama Blog inampa hongera sana Dada Bonnah Kaluwa kwani watanzania wanahitajia wanawake wenye kuthubutu na kusonga mbele kama wewe,hivyo tunakutakia kila la heri katika safari yako ya bungeni Dodoma.