Muigizaji
wa filamu za kibongo ambaye wiki iliyopita ameshinda tuzo ya muingizaji
bora wa kike katika tuzo za Filamu nchini Tanzania (TAFA) Irene Paul
amefunguka na kusema kuwa ameshatoa
mimba nyingi sana, Irene Paul alisema hayo alipokuwa akichat Live
katika kipengele cha KIKAANGONI kinachofanyika katika ukurasa wa
facebook wa EATV kila siku ya Jumatano kuanzia saa nane mchana mpaka
kumi Alasiri.
Irene
Paul alisema kuwa mara nyingi amekuwa akitoa mimba hizo katika filamu
kutokana na kuuvaa uhusika ili kufikisha ujumbe kwa jamii kama ambavyo
Scene inamtaka kufanya hivyo, lakini katika uhalisia hajawahi kufanya
jambo hilo.
"Irene
Bahati Paul, katika movie nimetoa mimba nyingi sana maana ndivyo
uhusika umenipasa kufanya hivyo ili kuwasilisha ujumbe katika jamii ila
kiuhalisia sijawahi kufanya hivyo."
Lakini
pia Irene Paul alizidi kuwachanganya mashabiki alipoulizwa juu ya kuwa
ana watoto wa ngapi na kusema kuwa ana watoto wengi sana hali ambayo
ilifanya mashabiki kutaka kujua watoto wengi kiaje na ni wanani na hapo
ndipo aliposema kuwa, yeye hata watoto ambao amewasaidia kuwalea
anawahesabu kama ni watoto wake, maana wamepata malezi yake na wao
wanamchukulia kama Mama yao.
"
Watoto nilionao wengi sana mpenzi, kuanzia niko shule nilikuwa na adopt
watoto kishuleshule, na wale wote ninaowasaidia kwa njia moja au
nyingine wananichukulia kama Mama maana mimi ni mlezi wao."
Irene
Paul ambaye kwa sasa anaonekana kukubalika kutokana na ufanisi wake
katika kazi yake ya sanaa alisema kuwa katika maisha ya mahusiano na
mapenzi amekutana na changamoto mbalimbali hususani kama kutendwa sababu
na yeye ni binadamu kama walivyo binadamu wengine, kwa sasa adai
hajaolewa na kuongeza kuwa kwa wakati huu wa sasa hafikiri kutafuta Mume
wala mchumba ila anajipanga tu kusambaza kazi zake tofauti na sanaa.
"
Mimi ni kama binadamu wengine napitia yote kama mwanadamu mwingine wa
kawaida katika maisha, kwa sasa jibu langu ni sitafuti mume wala mchumba
najitayarisha kusambaza kazi yangu tofauti na sanaa, kisanaa najipanga
kutoka katika ubora zaidi maana baada ya kuona mapokezi na apreciation
za wataNZAnia nadhani wananidai zaidi ya ninavyowapa".
Ukiachia
mbali juu ya sanaa yake Iren Paul amesema kuwa anatamani kuona yeye
amekuja daraja ambapo watu watamkumbuka kwa mchango wake wa mawazo,
maneno au vitendo hata kimali ili mradi tu atumike katika kufanya jambo
hilo.
"Katika
maisha yangu yajayo natamani kuwa daraja ambalo siku moja mtu
atalikumbuka na kusema ni kwa sababu ya lile au yule nimefika nitakako
yaani iwe kwa mawazo maneno au vitendo, kihali au kimali ili mradi tu
nitumike"
Lakini
pia muigizaji huyo wa bongo movie alimaliza kwa kutoa darasa kwa
baaadhi ya watu wanaohitaji kujiunga katika tasnia ya filamu Tanzania na
kuwaambia kuwa kila jambo linahitaji malengo na mipango huku ukitambua
unafanya nini lakini akadai atatoa darasa kupitia semina mbalimbali
atakazoandaa ili kuwasaidia watu wanaohitaji kuingia katika tasnia hiyo.
"Nitawapa
semina mbalimbali kupitia mikutano midogomidogo nItakayoiandaa hivi
karibuni na kutembelea shule mbalimbali kuwatia moyo wale wenye nia ya
kufika mbali lakini kwa wale ambao wanahitaji kujiunga katika tasnia
kwanza jua unataka uigizaji kwa sababu gani,halafu weka malengo yako na
uyaamini kwa kuyatekeleza,njia ni kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha
unaifanya kwa ubora pale upatapo nafasi ,thamini kidogo ulichonacho
maana kupitia hicho utapata kikubwa utakacho"
CREDITS:EATV
0 Comments