I was single once, but now i'm a wife and a mother. Nimekaa nikaona
siovibaya iwapo nta-share tips kadhaa zilizonisaidia kumuweka baba
watoto sawa na mpaka leo hii sijawahi kuhisi wala kugundua kwamba
anatoka nje ya ndoa yetu, japo matatizo ya hapa na pale hayakosekani ila
tumedumu na bado tunaendelea nasafari.Unapokutana na mwanaume
akakutongoza/mwanamke akakukubalia kuna uwezekano mkubwa kuwa amevutiwa
na wewe kweli au kakutamani tu. Kitu ambacho watu hua wanasahau ni
kwamba hata mtu aliyekutamani tu unaweza ukampa mwongozo/sababu mpaka
mwenyewe akajikuta anakupenda kuliko ambavyo angeweza kutarajia kwamba
angewahi kupenda. Ndio maana hata wale waitwao 'bad girls/boys' hua
wanajikuta wamenaswa na kunasika at some point.1. Usiigize.Maigizo
waachie wasanii wetu, kuwa vile ulivyo kweli kimaisha/kitabia (isiwe
mbaya)/mazoea n.k2. Don't move too fast/act desperate.Usitumie ule muda
wa mwanzo kabisa wa mahusiano yenu kutaka kujua "una malengo gani
namie?" "utanioa?" "Kanitambulishe/nataka nikakutambulishe." n.k Mpe
nafasi ya kukusoma na kupata kujua wewe ni mtu wa aina gani, je
unafanania na mwanamke ambae angependa kuwa nae kwa muda mrefu, possibly
hata ndoani? Na wewe nawe tumia muda huo kufanya kitu hicho
hicho.3.Don't be too demanding.Huyo sio baba yako wala sio mume just
yet, hivyo chochote atakachokufanyia kinatokana na yeye kutaka/kupenda
kufanya hivyo na sio kwakulazimika. Haki hiyo hauna.4. Kuwa na
shukurani.Learn to appreciate all that he does for you, that wayataona
umuhimu wa hayo anayokufanyia, yawe makubwa au madogo.5. Be real.Badala
ya kufika kwake na kuanza kushangaa anaishije bila ya mfanyakazi wa
ndani huku ukitamba kuwa wewe huwezi, shangaa anawezaje weka nyumba yake
katika hali nzuri mwenyewe bila ya msaada. Hii itaonyesha fika wewe
utakua mke wa aina gani hapo baadae, kama ni wale wakukaa miguu juu huku
wakiagiza hata maji waliyoombwa na mume au la.6. Learn to cook if you
don't know how to.Waliosema "the way to a man's heart is through his
stomach" hawakukosea. Ukiachilia mbali wale watu wachache wanaokula ili
kushiba wengi hua wanajaliladha. Hiyo ndio hua inawaongezea hamu ya kula
na kuwarudisha nyumbani mapema pia kuwafanya wakumiss pale
inaposhindikana kula chakula chako. Kwakumwonyesha mwanaume kwamba hata
tumbo lake unaweza kuliridhisha unamwongezea sababu za kukuweka kwenye
maisha yake.7. Mheshimu.Mpe heshima yake kama mwanaume wako ila
usimwogope. Wengine wote usiwape nafasi kumfanya ajisikie kwamba
haheshimiki.8. Kuwa ngao yake.Inapotokea anakumbwa na matatizo yoyote
yale onyesha utayari wa wewe kuwa pamoja naye kwa hali na mali mpaka
yatakapoisha. Pia usikose kumjali kumpa moyo pale unapoona
inahitajika.9. Kuwa muwazi.Kama kuna mambo ambayo unajua moja kwa moja
yatakuwa sehemu ya mahusiano yenu (watoto/X mkorofi .nk) mweleze mapema
ili aamue kama yuko tayari kudeal nayo au la.10. Usiwe na chuki.Kikifika
kipindi cha yeye kukutambulisha kwa ndugu na rafiki zake onyesha
ushirikiano. Usionyeshe chuki wala kujiona kana kwamba wewe ndio
wewe.11. Give your all.Kama na nyie mtaamua kuonjeshana tunda kabla
(kama ambavyo wengi wanafanya karne hii) basi kuwa mbunifu, mtundu na
usiwe mvivu.12.Pendeza.Vaa/onekana vizuri unapokuwa nje hata ndani pia.
Usisahau kuzingatia/jali hisia zake kuhusu mavazi yako.13. Onyesha
interest kwa yale ayapendayo yeye.Usiwe mbinafsi kila siku unataka
kusikilizwa wewe tu na story/mambo utakayo wewe. Uliza/jua kuhusuyale
anayopenda yeye mf. mpira/siasa.14.Kuwa mtulivu.Usiwe mtu ambae kila saa
simu yako inapigwa pigwa na wanaume wasio ndugu wala marafiki wakaribu
na wanaoeleweka. Discpline ni muhimu sana.15.Usimzonge.Usiwe mmoja wa
wale watu wanaofuatilia wenzi wao masaa yote wanapokuwa hawapo pamoja.
Mpenafasi ya kuwa na marafiki zake bila kuhitaji kuzimasimu ama
ku-ignore simu/text zako.
With my Brothers in Leadership...
-
Asanteni Kaka Zangu,naendelea kujifunza kwenu.
(Mimi,DC Simalenga na DC Mchopanga)
1 week ago
0 Comments