Ticker

10/recent/ticker-posts

JE?.. ULIWAHI KUVUTIWA NA UVAAJI WA PHARRELL WILLIAMS, BASI ILE STYLE YAKE IMEMPA TUZO..!!

pharrell-williams-coachella-650-430
Hii inamfanya awe HAPPY kwakweli.. wapo walioshangaa pia kwamba yani kweli Tuzo hii inaenda kwa Pharell..?
Staa huyo wa muziki alikuwa kwenye Headlines ya story ambazo hazikuwa poa sana ndani ya mwezi huu kutokana na ishu ya kushtakiwa na kukutwa na hatia ya kukopi wimbo waMarvin Gaye.
Nyingine ambayo huenda hujaipata ni ishu ya Pharell Williams kutajwa kuwa ndiye mwanamuziki aliyeshinda CFDA Fashion Icon Awards ambapo ushindi huo unatokana na jinsi style yake imekuwa maarufu na kushawishi watu wengi duniani.
pharellwilliams759
Pharell atapewa Tuzo hiyo June 1 2015, lakini toka jina lake limetajwa kama mshindi mitandao imeendelea kuandika na kuuchambua huu ushindi wa Pharell.. wapo walioandika eti kawa mshindi kwa sababu ya ile kofia ambayo anapendelea kuvaa!
Mastaa wengine waliowahi kushinda Tuzo hii ni pamoja na Rihanna na Lady Gaga.
Pharrell-Williams-lands-Fashion-Icon-Awards-from-CFDA
Unaweza kuniandikia comment yako mtu wangu, eti Pharell anastahili hii Tuzo kutokana na kuvaa kwake?