Ticker

10/recent/ticker-posts

HAWA NDIO MASTAA 10 WA SOKA MATAJIRI ZAIDI DUNIANI...

soccer-start-and-restart-of-play 
Cristiano Ronaldo ameendelea kuudhihirishia ulimwengu kwamba mbali ya kuwa bora kwenye soka, bado ana rekodi nyingine kubwa ambazo zinafanya jina lake kuwa kwenye rekodi mbalimbali ambazo zitadumu milele duniani.

Takwimu za mtandao wa goal.com
 zinaonyesha staa huyo kuwa NUMBER 1 kwenye orodha ya mastaa wa soka wanaoongoza kwa kuingiza pesa nyingi zaidi duniani na kuwa na utajiri mkubwa.

Takwimu za mtandao huo zinaonyesha Ronaldo ana utajiri wa paundi milioni 210 akimuacha nyuma mpinzani wake anayeshikilia nafasi ya pili Lionel Messi mwenye utajiri wa paundi 200.

Utajiri wa Ronaldo haupatikani kwa soka lake uwanjani pekeyake, ana madili mengine mengi ikiwemo kuwa balozi wa kampuni mbalimbali kama Toyota, Nike na  Herbalife ambazo zimeweka pesa kwa staa huyu ili awe Balozi wao rasmi kutangaza bidhaa zao.

Hii ndio list yote.
1. Cristiano Ronaldo
ronaldo
Mchezaji wa Real Madrid: Huyu ndiye mchezaji bora wa dunia na ameendelea kushikilia rekodi yake ya nafasi ya kwanza, ana utajiri wa Euro milioni 210
2. Lionel Messi
messi
Ni mchezaji wa Barcelona: ana utajiri wa Euro milioni 200
3. Neymar Da Silva Santos Jr
neymar
Staa wa soka toka Brazil ambaye anachezea klabuya Barcelona: Utajiri wa Euro milioni 135
4. Zlatan Ibrahimovic
zlatan
Striker wa Klabu ya Paris Saint- German Fc: Ana utajiri wa Euro milioni 105
5. Wayne Rooney
roo
Mshambuliaji wa muda mrefu Klabu ya Manchester United: Utajiri wake ni Euro milioni 103
6. Ricardo Kaka
kaka
Ni kiungo wa timu ya Taifa ya Brazil na Orlando City: Ana utajiri wa Euro milioni 96
7. Samuel Eto’o
hb etoo
Jamaa anachezea Klabu ya U.C Sampdoria: Utajiri wake ni Euro milioni 87
8. Raul Gonzalez
raul
Mshambuliaji wa timu ya Al Sadd SC: Ana utajiri wa Euro 85
9. Ronaldinho (Gaucho)
ronaldno
Ni kiungo wa Queretaro F.C: Ana utajiri wa Euro milioni 83
10. Frank Lampard

Ni kiungo wa Manchester City: Ana utajiri wa Euro milioni 80