Ticker

10/recent/ticker-posts

WAZIRI SAMWEL SITTA AMSIMAMISHA KAZI BOSI BANDARINI



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA UCHUKUZI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI -

Nimemsimamisha kazi kwa Muda Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Ndgu.Madeni Kipande leo hii trh 16 Februari 2015 ili kupisha uchunguzi unaohusu tuhuma mbalimbali zinazomkabili.
Tuhuma hizo ni Pamoja na manung'uniko kuhusiana na ukiukwaji wa taratibu za manunuzi .Hali hii inatokana na kutotabirika kwa taratibu na kukosekana kwa uwazi , pamoja na taratibu hizo kuingiliwa na mamlaka.
Aidha tuhuma nyingine ni mahusiano yasiyoridhisha kati ya Uongozi wa Mamlaka ya Bandari na wadau wake muhimu na Mahusiano mabaya sehemu ya kazi.
Kufuatia hali hii,nimeteua Tume ya kuchunguza suala hili na nimeipa muda wa wiki mbili Kukamilisha kazi hii na kunipatia taarifa. Majina ya Tume hiyo ni Kama ifuatayo :-
1.Jaji Mstaafu Agusta Buheshi-Mwenyekiti.
2.Ndgu.Ramadhan Mlingwa-Mjumbe
3.Eng.Samson Luhigo-Mjumbe
4.Ndgu.Happiness Senkoro-Mjumbe
5.Ndgu.Flavian Kinundo -Mjumbe
6.Ndgu.Deogratius Kasinda-
Katibu
Wakati Ndgu.Kipande akiwa amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi, kwa mujibu wa Mamlaka niliyopewa na sheria ya Bandari Namba 17 ya Mwaka 2004 Kifungu Cha 34 Kifungu kidogo cha 2 ninamteua Meneja wa Bandari Dar Bwana Awadh Massawe kukaimu nafasi hiyo kuanzia leo trh 16 Februari 2015.

Samuel Sitta (Mb)
Waziri wa Uchukuzi.
16 Februari 2015.