Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ akiwa mapajani mwa Mbongo Fleva, Raheem Rummy Nanji ‘Bob Junior'.
LICHA ya
Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ kuwahi kufikishwa kortini
na Mbongo Fleva, Raheem Rummy Nanji ‘Bob Junior, wamebambwa ‘live’
wakioneshana mahaba niue, Amani lina tukio zima.
Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ akizidi kupozi kimahaba na ‘Bob Junior'.
TUJIUNGE TEGETA, DAR
Ishu hiyo iliyopigwa
chabo na paparazi wetu hivi karibuni lilijiri ndani ya Ukumbi wa Club 71
uliyopo Tegeta jijini Dar es Salaam ambapo Wema siku hiyo
alimtambulisha msanii wake mpya anayesimamiwa na kampuni yake ya Endless
Fame anayeitwa Ally Luna.
WAKUTANA
Katika tukio hilo, Wema ndiye aliyeanza kufika ukumbini humo akifuatana na timu yake, akiwemo Petit Man (kama kawa).
Muda mfupi baadaye, Bob
Junior naye alifika ambapo alipokutana na Wema walianza kupeana mahaba
huku wakigandana kwa zaidi ya dakika kumi.
Mbali na Bob Junior, Wema
alialika wasanii kibao kwa ajili ya kumsapoti ambao hata wao walipigwa
butwaa baada ya kushuhudia tukio hilo.
Wakiwa katika chumba cha VIP, Wema aliendelea kuwa ‘veri klozi’ na Bob Junior hivyo kusababisha minong’ono ya hapa na pale.
MAPOZI
Katika tukio hilo,
kilichowashangaza mashuhuda zaidi ni kitendo cha Wema kukaa mapajani kwa
Mbongo Fleva huyo bila kujalia macho ya watu.
Wema Sepetu na ‘Bob Junior' wakiteta jambo.
SALAMU KWA DIAMOND NA ZARI?
Baadhi ya mashuhuda wa
tukio hilo walikwenda mbali zaidi na kuanza kuhisi tabia hiyo ya Wema na
Bob Junior ni salamu kwa aliyekuwa mwandani wake na kumwagana Nasibu
Abdul ‘Diamond’ na ‘bebi’ wake wa sasa, Zarinah Hassan ‘Zari’.
“Hapa naona kama
sielewielewi maana ni mara ya kwanza kumwona Wema na Bob Junior
wakigandana kiasi hiki tangu walipopelekana mahakamani kipindi kile na
ukizingatia Sharobaro (Bob Junior) alikuwa hasimu wa Diamond aliyekuwa
mpenzi wa Wema kipindi hicho,” alisema mmoja wa mastaa wakubwa (jina
linahifadhiwa). Akaongeza:
Wema Sepetu akimchumu ‘Bob Junior.
“Nakuhakikishia hizi ni salamu kwa Diamond na yule Zari wake. Hapa Wema anajua kabisa salamu zitawafikia.”
Baadhi ya mastaa hao
walionekana kulaani tukio hilo na kujaribu kumtahadharisha Wema juu ya
ukaribu huo kwani kama Diamond atagundua atajua ni ishu za kulipizana
visasi.
“Kwa vyovyote Diamond
akigundua jambo hili litamfanya ukaribu wake na Wema kuzidi kuwa mgumu
na kuurejesha ni ndoto kama wana mpango wa kurudiana.”
WENYEWE WANASEMAJE?
Paparazi wetu alipojaribu
kuwadodosa wawili hao juu ya uhusiano wao, kila mmoja aliishia kucheka
tu bila kutoa majibu ya kueleweka.
DAKTARI AMUONYA WEMA
Wakati huohuo, mmoja wa
madaktari wa mastaa Bongo (jina lipo) amemuonya Wema kuhusu masuala ya
mapenzi kwamba, kama ni kweli ameanzisha uhusiano mwingine si vizuri
kwani bado akili yake haijatulia tangu amwagane na Diamond hivyo
anahitaji muda ili kutuliza akili.
“Wema hatakiwi kuanzisha uhusiano wa kimapenzi kwa haraka, wala si
vizuri kulipiza kisasi kwani anaweza kujikuta pabaya zaidi, haya mambo
ya mapenzi yanatesa sana mastaa wengi na nimekuwa nikiwapa huduma za
kisaikolojia,” alisema dokta huyo kwa sharti la kutotajwa gazetini.
TUJIKUMBUSHE
Mwaka 2011, Mahakama ya
Mwanzo Kinondoni jijini Dar ilimhukumu Wema kwenda jela miezi sita au
faini ya shilingi elfu 40 baada ya kupatikana na hatia ya kumtukana
matusi ya nguoni Bob Junior ambapo alilipa faini na kuachiwa huru jambo
lililoibua uhasama mkubwa kati yao.
Hivyo, tukio la kuonekana pamoja na kugandana kimahaba ni ishara njema kuwa sasa wapo vizuri na ule uhasama haupo tena!!